Hadithi

Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «بَدَأَ الْإِسْلَامُ غَرِيبًا، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا، فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Uislamu ulianza ukiwa kwa mtu mmoja mmoja na uchache wa watu wake, na utarejea ukiwa mgeni kwa uchache wa wenye kuutekeleza kama ulivyoanza, twawatamani, na uzuri ulioje kwa wageni, na furaha na kitulizo cha jicho kwao.

Mafunzo

  • Habari kuhusu kutokea ugeni wa Uislamu baada ya kuenea kwake na umaarufu wake.
  • Hapa kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yatakayotokea baada yake, na ikatokea kama alivyoeleza.
  • Fadhila ya atakayehama nchi yake na familia yake; na kwamba atakuwa na Pepo.
  • Wageni ni wale wanaotengemaa watu wanapoharibika, nao ni wale wanaorekebisha yale waliyoyaharibu watu.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الإسلام بدأ غريبًا في آحاد من الناس وقلّة أهله، وسيعود غريبًا بقلة من يقوم به كما بدأ، فغِبطةٌ، ونعمَ للغرباء، وفرحٌ وقرةُ عين لهم.

  • الإخبار بوقوع غربة الإسلام بعد انتشاره واشتهاره.
  • فيه علمٌ من أعلام النبوة، حيث أخبر النبي صلى الله عليه وسلم بما سيقع بعده، فوقع كما أخبر به.
  • فضل من هجر أوطانه وعشيرته؛ لأجل الإسلام، وأن له الجنة.
  • الغرباء هم الذين يَصلحون إذا فسد الناس، وهم الذين يُصلحون ما أفسد الناس.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi