Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Ni nzuri (Hasan)Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَادمِ اللَّذَّاتِ» يَعْنِي الْمَوْتَ.
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo.
Ufafanuzi
Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kukithirisha kukikumbuka kifo ambacho kukikumbuka kwake mtu anakumbuka Akhera, na kunabomoa mapenzi yake ya kupenda ladha za dunia ndani ya moyo wake, na hasa hasa zile za haramu.
Mafunzo
- Kifo kinakata ladha za dunia, lakini kwa muumini kinamuhamisha kwenda katika ladha za Akhera na ladha za pepo na yale yanayopatikana ndani yake miongoni mwa kheri kubwa.
- Kukumbuka kifo na yale yanayokuwa baada yake ni miongoni mwa sababu za kutubia na kujiondoa katika dhambi na kujiandaa na Akhera.
Ufafanuzi: العربية
حثَّ النبي صلى الله عليه وسلم على الإكثار من تذكُّر الموت الذي بذكره يتذكر الإنسان الآخرة، و تهدم محبته لذات الدنيا في قلبه، وخاصة المحرّمة.
- الموت يقطع لذَّات الدنيا، ولكنه في حقِّ المؤمن ينقله إلى لذَّات الآخرة ولذَّات الجنة وما يحصل فيها من الخير العظيم.
- تذكر الموت وما بعده من أسباب التَّوبة والإقلاع والاستعداد للآخرة.