Hadithi

Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنَّ اللهَ يَرْضَى لَكُمْ ثَلَاثًا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ ثَلَاثًا، فَيَرْضَى لَكُمْ: أَنْ تَعْبُدُوهُ، وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَأَنْ تَعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ: قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ الْمَالِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu anapenda kwa waja wake mambo matatu, na anachukia kutoka kwao mambo matatu, anapenda kutoka kwao: Wampwekeshe yeye pekee na wala wasimshirikishe na chochote, na washikamane na ahadi ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na mafundisho ya Nabii wake wote, na wala wasifarakane katika umoja wa Waislamu. Na anachukia kwao: Upuuzi na maneno yasiyokuwa na faida katika yale yasiyowahusu, na kuuliza jambo ambalo bado halijatokea, au kuwaomba watu mali zao, na vile wanavyovimiliki, na yale yasiyokuwa na ulazima wa kuyaomba, na kupoteza mali na kuzitumia katika njia zisizokuwa za kisheria, na kuziweka katika uharibifu.

Mafunzo

  • Anapenda Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoka kwa waja wake utakasifu katika ibada zake, na anachukia kumkufuru.
  • Himizo la kushikana katika kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa ndani yake kuna umoja na maelewano.
  • Himizo la umoja, na amri ya kushikamana nao na kuziweka pamoja safu zake, na katazo la kinyume chake kama kufarakana na kuhitilafiana.
  • Katazo la kukithirisha maneno kwa yale yasiyomuhusu; kwa sababu yakiwa ni ya halali basi ndani yake kuna kupoteza wakati, na yakiwa ya haramu basi kutakuwa na madhambi mengi.
  • Katazo la kujiingiza katika habari za watu na kufuatilia hali zao na kusimulia kauli zao na matendo yao.
  • Katazo la kukithirisha maswali katika mambo ya watu.
  • Uharamu wa kupoteza mali, na himizo la kuzihifadhi na kuzitumia katika yale yanayofaa.
Ufafanuzi: العربية

أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الله يحب من عباده ثلاث خصال، ويكره منهم ثلاثًا، فيحب منهم: أن يوحدوه ولا يشركوا به شيئًا، وأن يعتصموا بعهد الله والقرآن وسنة نبيه جميعًا، ولا يتفرقوا عن جماعة المسلمين. ويكره لهم: اللغو وفضول الكلام فيما لا يعنيهم، والسؤال عما لم يقع، أو سؤال الناس أموالهم، وما في أيديهم، وما لم تدعو إليه حاجة، وإضاعة المال وصرفه في غير وجوهه الشرعية، وتعريضه للتلف.

  • يحب الله تعالى من عباده الإخلاص في عبادته، ويبغض الكفر به.
  • الحض على الاعتصام والتمسك بحبل الله تعالى؛ لما فيه من اجتماع وائتلاف.
  • الحث على الجماعة، والأمر بلزومها وتوحيد صفوفها، والنهي عن ضدها من التفرق والاختلاف.
  • النهي عن كثرة الكلام بما لا يعني؛ لأنه إن كان مباحًا ففيه إضاعة الوقت، وإن كان حرامًا ففيه كثرة المآثم.
  • ترك الخوض في أخبار الناس وتتبع أحوالهم وحكاية أقوالهم وأفعالهم.
  • النهي عن كثرة السؤال لأموال الناس.
  • تحريم إضاعة المال، والحث على المحافظة عليه فيما ينفع.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi