Hadithi

Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Bukhari na Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ صَخْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْت رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم يَقُولُ: «مَا نَهَيْتُكُمْ عَنْهُ فَاجْتَنِبُوهُ، وَمَا أَمَرْتُكُمْ بِهِ فَافْعَلُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ، فَإِنَّمَا أَهْلَكَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ كَثْرَةُ مَسَائِلِهِمْ، وَاخْتِلَافُهُمْ عَلَى أَنْبِيَائِهِمْ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira Abdul-Rahman bin Swakhar -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Yale niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi fanyeni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao".

Ufafanuzi

Ametubainishia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa atakapotukataza kitu basi ni wajibu juu yetu kukiacha pasina kubagua, na atakapotuamrisha kwa chochote basi ni juu yetu kukifanya kile tunachokiweza. Kisha akatutahadharisha ili tusije kuwa kama baadhi ya umma zilizopita pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume nao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa aina mbali mbali za maangamivu na uharibifu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.

Mafunzo

  • Hadithi ni kanuni katika kubainisha kuwa la wajibu ni kutekeleza amri na kujiepusha na makatazo.
  • Katazo halikuruhusu kufanya chochote katika hayo, lakini amri imewekwa sharti la uwezo; kwa sababu kuacha ni jambo liko ndani ya uwezo na kufanya kunahitaji uwezo wa kuleta kitendo kilichoamrishwa.
  • Katazo la kuuliza maswali mengi Wanachuoni wamegawanya kuuliza katika sehemu mbili: Moja wapo: Ni maswali yanayokuwa katika mfumo wa kujifunza yale anayoyahitajia mtu kuhusiana na mambo ya dini, hili limeamrishwa, na miongoni mwa aina hii ni maswali ya Maswahaba, na aina ya pili: Ni maswali yanayokuwa katika sura ya kiburi na kujikalifisha, na hii ndiyo iliyoharamishwa.
  • Tahadhari kwa Umma huu dhidi ya kumpinga Nabii wake, kama ilivyotokea katika Umma zilizokuwa kabla yake.
  • Makatazo yanakusanya kidogo na mengi; kwa sababu haiwezekani kuyaepuka ila kwa kuyaepuka kidogo yake na mengi yake, kwa mfano: Ametukataza riba hii inakusanya ndogo yake na kubwa yake.
  • Kuacha sababu zinazopelekea katika haramu; kwa sababu hilo ni miongoni mwa maana za kuepeuka.
  • Haitakiwi kwa mtu atakaposikia amri ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake aseme: Je ni wajibu au ni sunna?, bali anawajibika kwenda mbio kutekeleza; kwa kauli yake: "Yafanyeni katika hayo kadiri muwezavyo".
  • Wingi wa maswali ni sababu ya kuangamia hasa hasa katika mambo ambayo haiwezekani kuyafikia, mfano kama mambo ya ghaibu, na namna ya hali ya siku ya Kiyama, usizidishe maswali ndani yake utaangamia, na ukawa ni king'ang'anizi na mtafuta mambo kwa undani.
Ufafanuzi: العربية

بين لنا رسول الله صلى الله عليه وسلم أنه إذا نهانا عن شيء وجب علينا اجتنابه بدون استثناء، وإذا أمرنا بشيء فعلينا أن نفعل منه ما نطيق. ثم حذرنا حتى لا نكون كبعض الأمم السابقة حينما أكثروا من الأسئلة على أنبيائهم مع مخالفتهم لهم فعاقبهم الله بأنواع من الهلاك والدمار، فينبغي أن لا نكون مثلهم حتى لا نهلك كما هلكوا.

  • الحديث قاعدة في بيان الواجب في إتيان المأمور واجتناب المحظور.
  • النهي لم يرخص في ارتكاب شيء منه، والأمر قيد بالاستطاعة؛ لأن الترك مقدور والفعل يحتاج إلى قدرة على إيجاد الفعل المأمور به.
  • النهي عن كثرة السؤال، قد قسم العلماء السؤال إلى قسمين: أحدهما: ما كان على وجه التعليم لما يحتاج إليه من أمر الدين، فهذا مأمور به ومن هذا النوع أسئلة الصحابة. والثاني: ما كان على وجه التعنت والتكلف وهذا هو المنهي عنه.
  • تحذير هذه الأمة من مخالفة نبيها، كما وقع في الأمم التي قبلها.
  • المنهي عنه يشمل القليل والكثير؛ لأنه لا يتأتّى اجتنابه إلا باجتناب قليله وكثيره، فمثلًا: نهانا عن الرِّبا فيشمل قليله وكثيره.
  • ترك الأسباب المفضية إلى المحرم؛ لأن ذلك من معنى الاجتناب.
  • لا ينبغي للإنسان إذا سمع أمر الرسول صلى الله عليه وسلم أن يقول: هل هو واجب أم مستحبّ، بل عليه بالمبادرة إلى الفعل؛ لقوله: «فَأْتُوا مِنْهُ مَا استَطَعْتُمْ».
  • كثرة المسائل سبب للهلاك ولا سيّما في الأمور التي لا يمكن الوصول إليها مثل المسائل الغيبية، وكيفية أحوال يوم القيامة، لا تكثر السؤال فيها فتهلك، وتكون متنطّعًا متعمّقًا.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi