Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ صُهَيْبٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا دَخَلَ أَهْلُ الْجَنَّةِ الْجَنَّةَ، قَالَ: يَقُولُ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: تُرِيدُونَ شَيْئًا أَزِيدُكُمْ؟ فَيَقُولُونَ: أَلَمْ تُبَيِّضْ وُجُوهَنَا؟ أَلَمْ تُدْخِلْنَا الْجَنَّةَ، وَتُنَجِّنَا مِنَ النَّارِ؟ قَالَ: فَيَكْشِفُ الْحِجَابَ، فَمَا أُعْطُوا شَيْئًا أَحَبَّ إِلَيْهِمْ مِنَ النَّظَرِ إِلَى رَبِّهِمْ عَزَّ وَجَلَّ».
Tafsiri
Na imesimuliwa kutoka kwa Suhaib Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Peponi, Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, atasema: "Je, mnataka kitu chochote niwazidishie?" Watasema: "Je, hukuziangaza nyuso zetu? Je, hukutuingiza Peponi, na ukatuokoa kutokana na Moto?" Kisha (Mwenyezi Mungu) atainua pazia, basi, hawatapewa kitu chochote kinachopendwa zaidi kwao kuliko kumwangalia Mola wao Mlezi Mwenye Nguvu, Mtukufu."
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa watakapoingia watu wa peponi peponi, Mwenyezi Mungu aliyetakasika na kutukuka atasema kuwaambia: Je, mnahitaji chochote nikuongezeeni? Watasema watu wa peponi wote kwa pamoja: Kwani hujazitia nuru nyuso zetu, kwani hujatuingiza peponi, na ukatuokoa na moto? Hapo, Mwenyezi Mungu Mtukufu ataondoa pazia na kulinyanyua; na pazia lake ni nuru, watajikuta hawajapewa kitu wanachokipenda zaidi kwao kuliko kumtazama Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
Mafunzo
- Kufunuliwa pazia kwa watu wa peponi, watamuona Mola wao, na ama makafiri; watazuiliwa na hilo.
- Neema kubwa zaidi ya peponi ni waumini kumuona Mola wao Mlezi.
- Watu wa peponi wote vyovyote vile zitakavyotofautiana daraja zao watamuona Mola wao Mlezi Aliyetakasika na kutukuka.
- Fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waumini kwa kuwaingiza peponi.
- Umuhimu wa kwenda haraka peponi kwa kutenda amali njema na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake.
Ufafanuzi: العربية
يُخْبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّه إذا دَخَلَ أهلُ الجَنةِ الجنةَ، يقول الله تبارك وتعالى لهم: هل تُريدون شيئًا أَزِيْدُكم؟ فيقول أهلُ الجنة كلُّهم: ألم تُبَيِّضْ وجوهَنا؟ ألم تدخلنا الجنة، وتنجِنا من النار؟ فيُزيلُ الله الحِجَابَ ويَرفعه؛ وحِجَابُه النُّور، فما أُعْطوا شيئًا أحبَّ إليهم من النَّظَر إلى ربِّهم عز وجل.
- كَشْفُ الحِجاب عن أهلِ الجَنة فيَرَون ربَّهم، وأما الكفار؛ فمَحْرُومون منها.
- أعظمُ نعيم الجنة رؤيةُ المؤمنين لربهم.
- كلُّ أهل الجنة مهما اختلفت منازلُهم سيرون ربَّهم جل وعلا.
- فضل الله على المؤمنين بإدخالهم الجنة.
- أهمية المسارعة إلى الجنة بالأعمال الصالحة وطاعة الله تعالى ورسوله صلى الله عليه وسلم.