Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ أَيِسَ أَنْ يَعْبُدَهُ الْمُصَلُّونَ فِي جَزِيرَةِ الْعَرَبِ، وَلَكِنْ فِي التَّحْرِيشِ بَيْنَهُمْ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Ibilisi amekwishakata tamaa waumini wenye kuswali kurudi kuabudu na kusujudia masanamu katika kisiwa Arab, lakini bado anatamaa, na bado nguvu zake na juhudi zake na harakati zake ziko katika kuwachochea baina yao kwa ugomvi na chuki na vita na fitina na mfano wa hayo.
Mafunzo
- Kumuabudu Shetani ni kuabudu sanamu, kwa sababu yeye ndiye muamrishaji na mshawishi wa hilo, kwa dalili ya kauli yake Mtukufu kuhusu Nabii Ibrahim -amani iwe juu yake- (aliposema): "Ewe baba yangu usimuabudu Shetani...."
- Shetani anakwenda mbio katika kuchochea ugomvi na chuki na vita na fitina baina ya waislamu.
- Miongoni mwa faida za swala katika Uislamu nikuwa inalinda mapenzi kati ya waislamu, na ikayatia nguvu mahusiano ya kiudugu baina yao.
- Swala ndiyo nembo kubwa ya dini baada ya shahada mbili, na ndio maana wameitwa waislamu wanaoswali.
- Kisiwa Arab kina mambo maalumu yasiyokuwepo katika miji mingine.
- Ikiwa kutasema kuwa, mbona kumetokea katika baadhi ya Kisiwa Arab ibada za masanamu, hali yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Hakika Shetani amekwishakata tamaa ya kuabudiwa na wenye kuswali...", hii ni taarifa ya yale yaliyotokea katika nafsi ya Shetani katika kukata tamaa baada ya kuona ufunguzi wa miji mbali mbali, na watu kuingia ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi, hadithi imeeleza dhana ya Shetani na kutokea kwake, kisha uhalisia ukawa kinyume na matarajio kwa hekima aliyoitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ إبليس أَيِسَ أنْ يَعُوْدَ المؤمنون المصلون لعبادته والسجود للصنم في جزيرة العرب، ولكنه لا زال يَطْمَع، ولا زال جهده وكَدُّه وعملُه وسعيُه في التَّحريش بينهم بالخصومات والشَّحْنَاء والحروب والفتن ونحوها.
- عبادة الشيطان عبادة الصنم، لأنه الآمِرُ به والداعي إليه، بدليل قوله تعالى عن إبراهيم عليه السلام: (يا أبت لا تعبد الشيطان…).
- الشيطان يَسعى في إيقاع الخصومات والشَّحْناء والحروب والفتن بين المسلمين.
- من فوائد الصلاة في الإسلام أنها تَحفظ المَوَدّة بين المسلمين، وتُقَوِّي روابط الأُخُوّة بينهم.
- الصلاة أعظم شعائر الدين بعد الشهادتين، ولذلك أطلق على المسلمين المُصَلِّين.
- جزيرة العرب لها خصائص دون غيرها من البلاد.
- إن قيل قد وقع في بعض جزيرة العرب عبادة الأصنام، والنبي صلى الله عليه وسلم يقول: (إن الشيطان قد أيس أن يعبده المصلون..)، فهذا إخبار عما وقع في نفس الشيطان مِن اليأس لِمَا رأى الفتوح، ودخول الناس في دين الله أفواجًا، فالحديث أخبر عن ظن الشيطان وتوقُّعِه، ثم كان الواقع بخلاف ذلك لحكمة يريدها الله عز وجل.