Hadithi

Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَمْرِو بْنُ سُلَيْمٍ الأَنْصَارِيُّ قَالَ: أَشْهَدُ عَلَى أَبِي سَعِيدٍ قَالَ: أَشْهَدُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «الغُسْلُ يَوْمَ الجُمُعَةِ وَاجِبٌ عَلَى كُلِّ مُحْتَلِمٍ، وَأَنْ يَسْتَنَّ، وَأَنْ يَمَسَّ طِيبًا إِنْ وَجَدَ».

Tafsiri

Kutoka kwa Amri Bin Suleim Al-Answari amesema: Ninamshuhudilia Abuu Saidi kuwa alisema: Ninamshuhudilia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa alisema: "Kuoga siku ya Ijumaa ni wajibu kwa kila aliyebaleghe, na apige mswaki, na aguse marashi ikiwa atapata".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kuoga siku ya Ijumaa kumetiliwa mkazo ni sawa na wajibu upande wa kila aliyebalehe katika waislamu waliowajibikiwa na Ijumaa, Na asafishe meno yake kwa mswaki na mfano wake, na ajitie manukato kwa harufu yoyote nzuri ya uturi.

Mafunzo

  • Kumetiwa mkazo kuoga siku ya Ijumaa kwa kila mwanaume wa kiislamu aliyebaleghe.
  • Usafi na kuondoa harufu mbaya ni jambo linalotakiwa na ni sheria kwa muislamu.
  • Kuitukuza siku ya Ijumaa, na kujiandaa kwa ajili yake.
  • Mkazo wa kutumia mswaki siku ya Ijumaa.
  • Sunna ya kujipaka manukato kwa harufu yoyote nzuri kabla ya kwenda katika swala ya Ijumaa.
  • Mwanamke akitoka nyumbani kwake kwa ajili swala ua kinginecho, haifai kwake kujitia manukato; kwa sababu mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yamekataza hilo.
  • Anayejiotea ni mtu aliyebaleghe, na kubaleghe hutokea kwa alama mbali mbali, tatu kati yake wanashirikiana wanaume na wanawake nazo ni: Ya kwanza: Kukamilisha miaka kumi na tano. Ya pili: Zikiota nywele pembezoni mwa tupu. Ya tatu: Kushusha manii kwa kujiotea au kwa matamanio au bila matamanio. Ama alama ya nne: Hii inamuhusu mwanamke, nayo ni: Hedhi, mwanamke akipata hedhi, anakuwa tayari kabaleghe.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ الغُسل يوم الجمعة مُتأكِّد كالواجب في حقِّ كلِّ ذَكَرٍ بالِغ من المسلمين ممّن وَجبت عليه الجمعة، وأن ينظِّف أسنانَه بالسواك ونحوه، وأن يتطيَّب بأيِّ رائحة عِطْرية طيبة.

  • تأكُّد استحباب غُسل يوم الجمعة على كلِّ رجل مسلم بالغ.
  • النَّظافة وإزالة الروائح الكَريهة مطلوبة شرعًا للمسلم.
  • تعظِيم يوم الجمعة، والاستعداد له.
  • تأكيد استحباب الاسْتِيَاك للجمعة.
  • استحباب التطيُّب بأيِّ رائحة عطرية طيبة قبل الذهاب للجمعة.
  • المرأة إذا خرجت من بيتها للصلاة أو غيرها، فلا يجوز لها التَّطَيُّب؛ لدلالة السُّنة على تحريم ذلك.
  • المحتلم هو البالغ، والبلوغ يحصل بعلامات، ثلاث منها يشترك فيها الرجل والمرأة وهي: الأولى: إكمال خمس عشرة سنة، والثانية: إذا نَبَتَ الشعر الخشن حول الفرج، والثالثة: إنزل المني بالاحتلام أو بالشهوة ولو بغير احتلام، وأما العلامة الرابعة فهي تخص المرأة وهي: الحيض، فإذا حاضت المرأة صارت بالغة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi