Hadithi

Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo.

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Addaar- Alqutni

Matini ya Kiarabu

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «اسْتَنْزِهوا من البول؛ فإنَّ عامَّة عذاب القبر منه».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Hadithi Marfu'u: "Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo".

Ufafanuzi

Anatubainishia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika hadithi hii kuwa moja ya sababu za adhabu za kaburi, ni hii iliyoenea sana, nayo nikutojisafisha vizuri na kujitwaharisha kutokana na mkojo.

Mafunzo

  • Kuchunga juu ya kujisafisha na kujiweka mbali na mkojo, ili usimpate katika mwili wake wala nguo yake.
  • Lililo bora ni kufanya haraka kuosha mahala hapo, na kujitwaharisha baada ya kupatwa; ili asiambatane na najisi, ama uwajibu wa kuiondoa unakuwa wakati wa swala.
  • Nikuwa mkojo ni najisi, ukiupata mwili au nguo au sehemu, unapanajisisha; Hivyo haiswihi swala kwa hilo; kwasababu kujisafisha kutokana na najisi ni moja kati ya sharti zake.
  • Nikuwa kuacha kujisafisha kutokana na mkojo ni katika madhambi makubwa.
  • kuthibiti kwa adhabu za kaburini, nazo zimethibiti kwa Qur'ani na sunna na makubaliano ya wanachuoni.
  • Kuthibitisha malipo Akhera, Hivyo sehemu ya kwanza katika vituo vya akhera ni kaburi: Ima iwe ni kiwanja miongoni mwa viwanja vya pepo, au shimo katika mashimo ya moto.
Ufafanuzi: العربية

يبين لنا النبي صلى الله عليه وسلم في هذا الحديث أحد أسباب عذاب القبر، وهو الأكثر شيوعاً، ألا وهو عدم الاستنزاه والطهارة من البول.

  • الحرص على التنزه والابتعاد من البول، بأن لا يصيبه في بدنه ولا ثوبه .
  • الأفضل المبادرة بغسله، والطهارة منه بعد إصابته؛ لئلا تصاحبه النجاسة، أما وجوب إزالتها فيكون عند الصلاة.
  • أن البول نجس، فإذا أصاب بدناً أو ثوباً أو بقعة، نجسها؛ فلا تصح بذلك الصلاة؛ لأن الطهارة من النجاسة أحد شروطها.
  • أن ترك التنزه من البول من كبائر الذنوب.
  • ثبوت عذاب القبر، وهو ثابت بالكتاب والسنة والإجماع.
  • إثبات الجزاء في الآخرة، فأول مراحل الآخرة هي القبور، فالقبر: إما روضة من رياض الجنة، أو حفرة من حفر النار.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi