Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَهَى أَنْ يُسْتَنْجَى بِرَوْثٍ أَوْ عَظْمٍ، وَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَا تُطَهِّرَانِ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama au mfupa, na akasema: "Vitu hivyo havisafishi sawa sawa".
Ufafanuzi
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekidhi haja yake sawa iwe haja ndogo au kubwa, kustanji kwa mfupa wa mnyama au kinyesi chake na mabaki yake yaliyokauka; na akasema: Hivyo haviondoshi najisi, na wala havisafishi vizuri.
Mafunzo
- Kumebainishwa baadhi ya adabu za kukidhi haja na kustanji.
- Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama; kwa sababu: Ima ni najisi, au kwa sababu ni chakula cha wanyama wa Majini.
- Katazo la kustanji kwa mfupa; kwa sababu ima ni najisi, au ni chakula cha Majini wenyewe.
Ufafanuzi: العربية
نهى النبي صلى الله عليه وسلم مَن قضى حاجته من بول أو غائط أن يستَجْمِر بعظم الحيوان أو روثه وفضلاته الجافّة؛ وقال: إنها لا تزيل النجاسة، ولا تطهر منها.
- بيان بعض آداب الخلاء والاستنجاء.
- النهي عن الاستجمار بالروث؛ لأنه: إما نجس، وإما لأنه عَلَفُ دوابِّ الجن.
- النهي عن الاستجمار بالعظم؛ لأنه إما نجس، وإما لأنه طعام الجن أنفسهم.