Hadithi

Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ سَلْمَانَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ لَنَا الْمُشْرِكُونَ: إِنِّي أَرَى صَاحِبَكُمْ يُعَلِّمُكُمْ حَتَّى يُعَلِّمَكُمُ الْخِرَاءَةَ، فَقَالَ: أَجَلْ، إِنَّهُ نَهَانَا أَنْ يَسْتَنْجِيَ أَحَدُنَا بِيَمِينِهِ، أَوْ يَسْتَقْبِلَ الْقِبْلَةَ، وَنَهَى عَنِ الرَّوْثِ وَالْعِظَامِ وَقَالَ: «لَا يَسْتَنْجِي أَحَدُكُمْ بِدُونِ ثَلَاثَةِ أَحْجَارٍ».

Tafsiri

Kutoka kwa Salman radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Washirikina walisema kutuambia: Hakika mimi ninamuona jamaa yenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni kukidhi haja, akasema: Ndiyo, hakika yeye ametukataza kustanji mmoja wetu kwa mkono wake wa kulia, au kuelekea kibla, na akakataza kinyesi cha wanyama na mifupa, na akasema: "Asistanji mmoja wenu kwa chini ya mawe matatu".

Ufafanuzi

Amesema Salman Al-Faarisi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Washirikina walisema kwa kutukejeli: Hakika Nabii wenu anakufundisheni kila kitu, mpaka anakufundisheni namna gani mtakidhi haja zenu kama haja ndogo au kubwa! Akasema Salmaan: Ndiyo, ametufundisha adabu za kukidhi haja; na miongoni mwake ni kwamba alitukataza rehema na amani ziwe juu yake kustanjia baada ya kukidhi haja kwa mkono wa kulia, kwa kuulinda na najisi na kwa kuupa heshima, au kuelekea kibla wakati wa haja ndogo au kubwa, na akakataza kustanji kwa kinyesi cha wanyama na mabaki yake na mifupa yake, na asitosheke aliyekidhi haja katika kustanji kwa chini ya mawe matatu.

Mafunzo

  • Kumebainishwa kuenea na ukamilifu wa sheria ya Uislamu katika kila wanachokihitajia watu.
  • Kumebainishwa baadhi ya adabu za msalani na kustanji.
  • Uharamu wa kuelekea kibla wakati wa kukidhi haja ndogo au kubwa; kwa kauli yake: "Alitukataza" Na asili ya katazo ni uharamu.
  • Katazo la kustanji, au kutumia maji kwa mkono wa kulia; kwa sababu ya kuuheshimu.
  • Ubora wa mkono wa kulia kwa mkono wa kushoto; kwa sababu mkono wa kushoto hutumika kuondoa najisi na uchafu, na wa kulia ni kinyume na hivyo.
  • Uwajibu wa kuondoa najisi kwa maji au mawe, sawa sawa najisi iwe kidogo au nyingi.
  • Katazo la kustanji kwa chini ya mawe matatu; kwa sababu mawe chini ya matutu huwa hayatakatishi mara nyingi.
  • Kila kinachotimiza lengo la kujisafisha na kujitakatisha, basi kinafaa, bali alitaja mawe rehema na amani ziwe juu yake; kwa sababu ndio hutumika mara nyingi, na kila kitakachokuwa hivyo basi hakina maana.
  • Mapendekezo ya kuhitimisha kustanji kwa witiri, ikiwa kutakata kutakuwa kwa mawe manne basi itapendeza aongeze la tano, na hivyo hivyo; kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayestanji kwa mawe basi na afanye witiri".
  • Katazo la kustanji kwa kinyesi cha wanyama: ima ni kwakuwa ni najisi, au kwakuwa ni malisho ya wanyama wa Majini.
  • Katazo la kustanji kwa mifupa; kwakuwa ima ni najisi, au ni chakula cha majini wenyewe.
Ufafanuzi: العربية

قال سلمان الفارسي رضي الله عنه: قال المشركون لنا استهزاءً: إن نبيكم يعلمكم كل شيء، حتى يعلمكم كيف تقضون حاجتكم من بول أو غائط! فقال سلمان: نعم، علمنا آداب قضاء الحاجة؛ ومن ذلك أنه نهانا صلى الله عليه وسلم أن نستنجي بعد قضاء الحاجة باليد اليمنى صيانة لها من النجاسة وإكرامًا، أو نستقبل الكعبة عند البول أو الغائط، ونهى عن الاستجمار بروث البهائم وفضلاتها وبعظمها، وألّا يكتفي المُحدِث في الاستجمار بأقل من ثلاثة أحجار.

  • بيان شمول وكمال الشريعة الإسلامية في كل ما يحتاج الناس إليه.
  • بيان بعض آداب الخلاء والاستنجاء.
  • تحريم استقبال القِبلة أثناء البول أو الغائط؛ لقوله: "نهانا" والأصل في النهي التحريم.
  • النَّهْيُ عن الاستنجاء، أو الاستجمار باليد اليمنى؛ تكريمًا لها.
  • تَفضيل اليَد اليُمنى على اليُسرى؛ لأن اليَد اليُسرى تُستخدم لإزالة النَّجاسات والقَذَارات، واليُمنى لما عَدا ذلك.
  • وجوب إزالة النجاسة بالماء أو الأحْجَار، سواء قَلَّت النجاسة أم كَثُرت.
  • النَّهْي عن الاسْتِجْمَار بأقلَّ من ثلاثة أحَجار؛ لأن أقل من ثلاثة أحجار لا ينقي في الغالب.
  • كل ما يحصل به المقصود من التَّطهر والإنْقَاء، فإنه يجزئ، وإنما نَص صلى الله عليه وسلم على الأحجار؛ لأنها الغَالب وما كان كذلك فلا مفهوم له.
  • استحباب قطع الاستجمار على وتْر، فإذا حصل الإنقاء بأربع استحب أن يزيد خامسة وهكذا؛ لقوله صلى الله عليه وسلم: (من استجمر فليوتر).
  • النهي عن الاستجمار بالروث؛ لأنه: إما نجس، وإما لأنه علف دواب الجن.
  • النهي عن الاستجمار بالعظم؛ لأنه إما نجس، وإما لأنه طعام الجن أنفسهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi