Hadithi

Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُقْبَةَ بْنَ عَامِرٍ الْجُهَنِيَّ رضي الله عنه قَالَ: ثَلَاثُ سَاعَاتٍ كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَنْهَانَا أَنْ نُصَلِّيَ فِيهِنَّ، أَوْ أَنْ نَقْبُرَ فِيهِنَّ مَوْتَانَا: حِينَ تَطْلُعُ الشَّمْسُ بَازِغَةً حَتَّى تَرْتَفِعَ، وَحِينَ يَقُومُ قَائِمُ الظَّهِيرَةِ حَتَّى تَمِيلَ الشَّمْسُ، وَحِينَ تَضَيَّفُ الشَّمْسُ لِلْغُرُوبِ حَتَّى تَغْرُبَ.

Tafsiri

Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhani radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nyakati tatu alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitukataza kuswali ndani yake, au kuzika ndani yake maiti wetu: wakati linapoanza kuchomoza jua mpaka linyanyuke, na wakati linapofika kati kati mpaka lipinde, na wakati linapoanza kuzama mpaka lizame.

Ufafanuzi

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyakati tatu za mchana kutoswali ndani yake swala za sunna, au kuzikwa ndani yake maiti: Wakati wa kwanza: Wakati linapodhihiri jua kwa kuchomoza, na hii ni wakati wa mwanzo wa kuchomoza kwake mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki, na inakadiriwa kuwani robo saa takribani. Wakati wa pili: Pindi jua linapofika kati kati ya mbingu, linapokuwa halina kivuli upande wa Mashariki au Magharibi mpaka linapoondoka kutoka kati kati ya mbingu, na kikaonekena kivuli upande wa Mashariki, wakati ambapo unaanza wakati wa Adhuhuri, nao ni wakati mfupi mno; ambao ni kiasi cha dakika tano takribani. Wakati wa tatu: Linapopinda na likaanza kuzamia Magharibi mpaka lizame.

Mafunzo

  • Nyakati zilizokatazwa kuswali ndani yake kama ilivyoonyesha hadithi hii na hadithi nyinginezo, nazo ni: Wa kwanza: Baada ya swala ya Alfajiri mpaka jua linapochomoza. Wa pili: Wakati wa kuchomoza jua mpaka linyanyuke kiasi cha mkuki kwa mtazamo wa jicho; yaani: kiasi cha dakika kumi na tano takribani. Wa tatu: Anaposimama msimamaji wa mchana mpaka jua liondoke, na hii ni wakati ambao unakuwa hakijabakia kivuli kwa mwenye kusimama mchana, upande wa Mashariki wala Magharibi, na wameukadiria baadhi yao kuwa ni dakika tano takribani. Wa nne: Baada ya swala ya Lasiri mpaka jua lizame. Wa tano: Wakati jua linapokuwa la njano mpaka lizame.
  • Katazo la kuswali katika nyakati hizi tano zilizokatazwa, zinaondolewa hapo swala za faradhi na swala zenye sababu.
  • Katazo la kuchelewesha kuzika mpaka katika nyakati hizi tatu zenye muda mfinyu zilizotajwa katika hadithi, na kufaa kwake katika nyakati nyinginezo sawa iwe mchana au usiku.
  • Hekima na maana ya kukataza kuswali ndani ya nyakati hizi: Asili ni nikuwa muislamu anajisalimisha kwa amri za Mwenyezi Mungu, na anajiepusha na makatazo yake kwa ajili ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, na wala haachi kuabudu mpaka aone hekima au sababu ya kuamrishwa hivyo, au kukatazwa hilo, bali anatakiwa atii, na imekuja katika hadithi zingine hekima katika hilo: Ya kwanza: Nikuwa katika wakati wa mchana kabla ya kupinduka jua Jahanamu huwashwa muwako mkali. Ya pili: Na ama hekima ya kukatazwa swala wakati wa kuchomoza jua na wakati wa kuzama kwake, ni kujifananisha na washirikina, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza kwake na wakati wa kuzama kwake. Ya tatu: Na ama katazo la kuswali baada ya Alfajiri mpaka kuchomoza kwa jua, na baada ya Lasiri mpaka kuzama kwake, hii ni sehemu ya kuziba njia zinazopelekea katika mabaya; mpaka kumalizike kutojifananisha na makafiri, na waislamu wasijifananishe nao katika ushirikina wao, kwani wao hulisujudia jua wakati wa kuchomoza na wakati wa kuzama kwake.
Ufafanuzi: العربية

نهى النبي صلى الله عليه وسلم عن ثلاثة أوقات من النهار أن يُصلَّى فيهن صلاة التطوع، أو أن يُقبر ويُدفن فيهن الموتى: الوقت الأول: حين تطلع الشمس بازغة، وذلك عند أول طلوعها حتى ترتفع مقدار رُمْح، وهو يُقدّر بربع ساعة تقريبًا. والثاني: حين تتوسّط الشمس منتصف السماء، فلا يكون لها ظل من جهة المشرق أو المغرب إلى أن تزول عن وسط السماء، ويظهر الظل من جهة المشرق حيث يبدأ وقت صلاة الظهر، وهو وقت قصير؛ وهو بمقدار خمس دقائق تقريبًا. والثالث: حين تميل وتشرع الشمس في الغروب حتى تغرب.

  • الأوقات المنهي عن الصلاة فيها كما دلَّ عليه هذا الحديث والأحاديث الأخرى هي: أولاً: بعدَ صلاة الفجْر إلى طلوع الشمس، ثانيًا: عندَ طلوع الشمس حتى ترتفع قدْر رمح في رأي العين؛ أي: بمقدار خمسة عشرة دقيقة تقريبًا، ثالثًا: حين يقوم قائمُ الظهيرة حتى تزولَ الشمس، وذلك حين لا يبقَى للقائم في الظهيرة ظلٌّ في المشرق ولا في المغرِب، وقدَّره البعض بخمس دقائق تقريبًا، رابعًا: بعدَ صلاة العصْر حتى تغرُب الشمس، خامسًا: عندَ اصفرار الشمس حتى تغرُب.
  • النَّهي عن الصلاة في هذه الأوقات الخمسة المنهي عنها، يستثنى منه الفرائض وذوات الأسباب.
  • النهي عن تعمد تأخير الدفن إلى هذه الأوقات الثلاثة الضيقة المذكورة في الحديث، وجوازه في أي ساعة من ليل أو نهار.
  • الحِكمة من النهي عن الصلاة في هذه الأوقات: الأصلُ أنَّ المسلِم يستسلم لأوامِر الله، ويجتنب نواهيَه تعبُّدًا لله، ولا يتوقَّف عن التعبُّد حتى يطَّلعَ على الحِكمة أو العِلَّة مِن الأمر بكذا، أو النهي عن ذلك، بل عليه أن ينقاد، وقد ورد في أحاديث أخرى الحكم في ذلك: أولاً: أنَّ في وقت الظهيرة قُبيل الزوال يُوقد فيه على جهنم إيقادًا بليغًا، ثانيًا: وأمَّا الحِكمة من النهي عنِ الصلاة عندَ طلوع الشمس وعندَ غروبها، فهي مشابهة المشركين، فإنَّهم يسجدون للشمس عندَ طلوعها وعندَ غروبها، ثالثًا: وأمَّا النهي عنِ الصلاة بعدَ صلاة الفجْر إلى طلوع الشمس، وبعدَ صلاة العصْر إلى غروب الشَّمس، فمِن باب سدِّ الذريعة؛ حتى ينقطِع التشبُّهُ بالكفَّار، ولا يتشبه بهم المسلِم في شِرْكهم، فإنهم يسجدون للشمس عند طلوعها وغروبها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi