Hadithi

Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي الثَّوْبِ الوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقَيْهِ شَيْءٌ».

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali katika nguo moja kutoyaacha wazi mabega yake na shingo yake kiasi kwamba haweki chochote chenye kumsitiri; kwa sababu mabega mawili hata kama si uchi; ila kuyasitiri yanawezekana wakati wa kusitiri uchi, na ni jambo lililo karibu na kumheshimu na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusimama mbele yake katika swala.

Mafunzo

  • Inafaa kuswali katika nguo moja ikiwa itasitiri sehemu za wajibu kusitiriwa.
  • Inafaa kuswali katika nguo mbili, moja inasitiri juu ya mwili, na nyingine inasitiri chini yake.
  • Inapendeza na ni sunna mwenye kuswali awe katika muonekano mzuri.
  • uwajibu wa kufunika mabega mawili au moja ndani ya swala, akiweza kufanya hivyo, na imesemekana kuwa katazo ni la kujitakasa (mbele ya Mwenyezi Mungu).
  • Uchache wa yale waliyoyamiliki Maswahaba katika mali, mpaka utakuta mmoja wao hamiliki nguo mbili.
  • Amesema Imam Nawawi katika maana ya hadithi: Hekima yake nikuwa akijifunga chini na kukawa juu ya mabega yake hakuna kitu basi hatosalimika na kutofunuka uchi wake, tofauti na ambavyo atakaiweka sehemu ya nguo juu ya bega lake, na ni kwa sababu anaweza kuhitaji kuishika kwa mkono wake au mikono yake akashughulishwa na hilo, na ikampita sunna ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua chake, na kuinyanyua kwake pale ambapo ni sheria kuinyanyua, na mengineyo, kwa sababu ndani yake kuna kuacha kusitiri juu ya mwili na sehemu ya pambo, na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukueni pambo lenu katika kila msikiti" [Al-Araf: 31].
Ufafanuzi: العربية

نَهَى النبيُّ صلى الله عليه وسلم مَن صلّى في ثوب واحد عن أنْ يُجَرِّدَ عاتقيه ما بين الكتف والعنق بحيث لا يضع عليهما شيئًا يسترهما؛ لأن العاتقين وإن لم يكونا عورة، فإن سترهما أمكن في ستر العورة، وهو أقرب إلى إجلال الله تعالى وتعظيمه أثناء الوقوف بين يديه في الصلاة.

  • جواز الصلاة في الثوب الواحد إذا ستر ما يجب ستره.
  • جواز الصلاة في ثوبين، أحدهما يستر أعلى الجسم، والآخر يستر أسفله.
  • استحباب كون المُصلِّي على هيئة حسنة.
  • وجوب سَتر العَاتِقَين أو أحدهما في الصلاة، إذا أمْكَنه ذلك، وقيل النهي للتنزيه.
  • قِلّة ما في أيدي الصحابة رضي الله عنهم من المال، حتى إن بعضهم لا يملك ثَوبين.
  • قال النووي في معنى الحديث: حكمته أنه إذا ائتزر به ولم يكن على عاتقه منه شيء لم يؤمن أن تنكشف عورته، بخلاف ما إذا جعل بعضه على عاتقه، ولأنه قد يحتاج إلى إمساكه بيده أو يديه فيشغل بذلك، وتفوته سنة وضع اليد اليمنى على اليسرى تحت صدره، ورفعهما حيث شرع الرفع، وغير ذلك، لأن فيه ترك ستر أعلى البدن وموضع الزينة، وقد قال الله تعالى: { خُذُوا ‌زِينَتَكُمْ عِنْدَ كُلِّ مَسْجِدٍ } [الأعراف: 31].

Mada

Ripoti kosa

Zaidi