Hadithi

Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن ابنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم قال: «أُمِرْتُ أَنْ أَسْجُدَ عَلَى سَبْعَةِ أَعْظُمٍ: عَلَى الْجَبْهَةِ وَأَشَارَ بِيَدِهِ عَلَى أَنْفِهِ، وَالْيَدَيْنِ، وَالرُّكْبَتَيْنِ، وَأَطْرَافِ الْقَدَمَيْنِ، وَلَا نَكْفِتَ الثِّيَابَ وَالشَّعَرَ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Nimeamrishwa nisujudu kwa viungo saba, kwa paji la uso, na akaashiria kwa mkono wake katika pua yake, na mikono miwili na magoti mawili, na ncha za miguu miwili, na wala tusizikunje nguo na nywele".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu kamuamrisha wakati wa swala asujudu kwa viungo saba katika viungo vya mwili; navyo ni: Cha kwanza: Paji la uso: Nao ni ubapa wa uso ulioko juu ya pua na macho mawili, Na akaashiria -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa mkono wake katika pua yake, akieleza kuwa paji la uso na pua ni kiungo kimoja katika vile saba, na akitia msisitizo kwa mwenye kusujudu kuwa agusishe pua yake katika ardhi. Cha pili: na cha tatu: Ni mikono miwili. Cha nne na cha tano: Ni magoti mawili. Cha sita na cha saba: Ni vidole vya miguu miwili. Na akatuamrisha tusizifunge nywele zetu, au kuzikunja kunja nguo zetu katika ardhi wakati wa kusujudu kwa kuilinda ardhi (Isiguse paji la uso); bali tuziache mpaka zidondoke katika ardhi, ili zisujudu pamoja viungo.

Mafunzo

  • Uwajibu wa kusujudu katika swala juu ya viungo saba.
  • Karaha ya kukusanya nguo na nywele ndani ya swala.
  • Ni wajibu kwa mwenye kuswali atulizane ndani ya swala yake, na hii ni kwa kuweka viungo saba vya kusujudu juu ya ardhi, na atulizane hapo mpaka alete dua zote zilizopangwa na sheria.
  • Katazo la kufunga nywele hili ni maalumu kwa wanaume pasina wanawake; kwa sababu mwanamke ndani ya swala ameamrishwa kujisitiri
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بأنَّ اللهَ أَمَرَه عند الصلاة أنْ يَسجُدَ على سبعةٍ من أعضاء الجسم؛ وهي: أولاً: الجبهة: وهي: صفحة الوجه فوق الأنف والعينين، وأشار صلى الله عليه وسلم بيده إلى أنفِه، مُبَيِّنًا أن الجَبْهةَ والأنف عضو واحد من السبعة، وتأكيدًا على أنَّ الساجِد يُلامِسُ بأنفِه الأرضَ. العضو الثاني والثالث: اليدان. الرابع والخامس: الرُّكْبتان. السادس والسابع: أصابع القدمين. وأَمَرَنا أنْ لا نَربِطَ شعورنًا، أو نَجمعَ ثيابَنا بعضَها على بعض عند السجود على الأرض صيانةً لها؛ بل نُرسِلُها حتى تقع على الأرض، فتسجد مع الأعضاء.

  • وجوب السُّجود في الصلاة على الأعَضاء السَّبعة.
  • كراهية جَمْعِ وضَمِّ الثَّوب والشَّعَر في الصلاة.
  • يجب على المصلي أن يطمئن في صلاته، وذلك بأنْ يضع أعضاء السجود السبعة على الأرض، ويستقر عليها حتى يأتي بالذكر المشروع.
  • النهيُ عن كَفِّ الشَّعَرِ خاصٌّ بالرجال دون النساء؛ لأن المرأة في الصلاة مأمورة بالتستر.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi