Hadithi

Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما: سَأَلَ رَجُلٌ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، مَا تَرَى فِي صَلاَةِ اللَّيْلِ، قَالَ: «مَثْنَى مَثْنَى، فَإِذَا خَشِيَ الصُّبْحَ صَلَّى وَاحِدَةً، فَأَوْتَرَتْ لَهُ مَا صَلَّى» وَإِنَّهُ كَانَ يَقُولُ: «اجْعَلُوا آخِرَ صَلاَتِكُمْ وِتْرًا» فَإِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَمَرَ بِهِ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake-: Bwana mmoja alimuuliza Mtume Muhammad rehema na amani za Allah ziwe juu yake akiwa juu ya mimbari, waonaje kuhusu swala za usiku, akasema: "Ni rakaa mbili mbili, atapochelea Alfajiri aswali rakaa moja, iwe ni witri kwa aliyo swali" na yeye alikuwa akisema: "Fanyeni swala yenu ya mwisho iwe ni witri", kwa hakika Mtume rehema na amani za Allah zimshukie kaamrisha hivyo.

Ufafanuzi

Mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake naye akiwa anahutubia juu ya Mimbari: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nifundishe ni namna gani nitaswali usiku?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Utaswali na kutoa salamu katika kila rakaa mbili, ukihofia kuchomoza kwa Afajiri basi swali rakaa moja itakufanyia kuwa witiri rakaa zingine ulizoswali, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiusia kuifanya swala ya mwisho ya usiku kuwa ni witiri.

Mafunzo

  • Asili katika swala za usiku ni mtu atoe salamu katika kila rakaa mbili, nje na witiri.
  • Nikuwa swala za usiku hazina idadi maalumu; kwa kuwa tamko liliachwa wazi.
  • Amesema Nawawi: "Swala za usiku na mchana ni rakaa mbili mbili", hadithi hii inachukuliwa kama kubainisha kilicho bora zaidi, nayo ni atoe salamu katika kila rakaa mbili, na sawa sawa ziwe ni sunna za usiku na mchana, na ni sunna atoe salamu kwa kila rakaa mbili.
  • Amesema Nawawi: Hapa kuna ushahidi kuwa sunna ni kuifanya witiri kuwa swala ya mwisho wa usiku, na kwamba wakati wake unamalizika kwa kuchomoza Alfajiri, na ndio kauli mashuhuri katika madhehebu yetu, na ndivyo lilivyosema jopo la wanachuoni.
Ufafanuzi: العربية

سأل رجل النبي صلى الله عليه وسلم وهو يخطب على المنبر: يا رسول الله علمني كيف أصلي الليل؟ فقال صلى الله عليه وسلم: تصلي وتسلم من كل ركعتين، فإذا خفت طلوع الصبح فصلِّ ركعة توتر لك ما صليت، وإنه صلى الله عليه وسلم كان يوصي بجعل آخر صلاة الليل وترًا.

  • الأصل في صلاة الليل أن يسلِّم من كل ركعتين، في غير الوِتر.
  • أن صلاة الليل غير مُقيدة بعَدد؛ لإطلاق اللفظ.
  • قال النووي: "صلاة الليل والنهار مثنى مثنى"، هذا الحديث محمول على بيان الأفضل، وهو أن يسلم من كل ركعتين، وسواء نوافل الليل والنهار يستحب أن يسلم من كل ركعتين.
  • قال النووي: فيه دليل على أن السنة جعل الوتر آخر صلاة الليل، وعلى أن وقته يخرج بطلوع الفجر، وهو المشهور من مذهبنا، وبه قال جمهور العلماء.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi