Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «تَفْضُلُ صَلاَةُ الجَمِيعِ صَلاَةَ أَحَدِكُمْ وَحْدَهُ، بِخَمْسٍ وَعِشْرِينَ جُزْءًا، وَتَجْتَمِعُ مَلاَئِكَةُ اللَّيْلِ وَمَلاَئِكَةُ النَّهَارِ فِي صَلاَةِ الفَجْرِ» ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ: فَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: {إِنَّ قُرْآنَ الفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا} [الإسراء: 78].
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Imekuwa ni bora swala ya wengi kuliko swala ya mmoja wenu peke yake, kwa vipengele ishirini na tano, na hukusanyika Malaika wa usiku na Malaika wa mchana katika swala ya Alfajiri" Kisha anasema Abuu Huraira: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78].
Ufafanuzi
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba thawabu na malipo ya swala ya mtu katika jamaa pamoja na imamu ni bora kuliko swala ishirini na tano anazoziswali peke yake nyumbani kwake au sokoni kwake, kisha akataja rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika wa usiku na mchana hukusanyika katika swala ya Alfajiri, kisha anasema Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake akitoa ushahidi kwa hilo: Someni mkitaka: "Hakika Qur'ani ya Alfajiri hushuhudiwa" [Al-Israa: 78] Yaani: Qur'ani ya Alfajiri huishuhudia Malaika wa usiku na Malaika wa mchana.
Mafunzo
- Amesema bin Hajari: Hakika swala ya msikitini kwa jamaa inazidi swala ya nyumbani na sokoni kwa jamaa au mtu mmoja mmoja, ameisema kauli hiyo bin Daqiiq Al-Idd.
- Hapa kuna fadhila ya swala ya Alfajiri; kwa kufanywa pekee kukusanyika kwa Malaika ndani yake.
- Amesema bin Bazi: Ni wajibu kwa muumini awe na pupa ya kuhifadhi swala katika jamaa hata kama nyumba yake itakuwa mbali, ili aipate kheri hii kubwa.
- Amesema Nawawi katika kukusanya kati ya riwaya ya kwamba swala ya jamaa ni bora kuliko swala ya mtu mmoja kwa daraja ishirini na tano, na nyingine kwa daraja ishirini na saba: Na kukusanya kati ya kauli hizi mbili ni kwa sura tatu: Ya kwanza: Hazipingani, kwani kutajwa kidogo hakupingani na wingi, na maana ya idadi haizingatiwi kwa wasomi wa misingi ya sheria. Ya pili: Yawezekana alieleza kidogo kisha Allah Mtukufu akamjulisha ziada ya fadhila, naye akaieleza. Ya tatu: Nikuwa zinatofautiana kulingana na kutofautiana kwa wenye kuswali, baadhi yao wanakuwa na ishirini na tano, na baadhi yao ishirini na saba kulingana na ukamilifu wa swala na kuihifadhi kwake na muonekano wake na utulivu wake na wingi wa mkusanyiko wake na ubora wao na utukufu wa eneo na mfano wa hayo, na Allah ndiye mjuzi zaidi.
Ufafanuzi: العربية
بيَّن النبي صلى الله عليه وسلم أن ثواب وجزاء صلاة الرجل في جماعة مع الإمام أفضل من خمس وعشرين صلاة يصليها وحده في بيته أو سوقه، ثم ذكر صلى الله عليه وسلم أن ملائكة الليل والنهار يجتمعون في صلاة الفجر، ثم يقول أبو هريرة رضي الله عنه مستشهدًا لذلك: فاقرءوا إن شئتم: {إِنَّ قُرْآنَ الفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا} [الإسراء: 78]، أي: إن صلاة الفجر تشهدها ملائكة الليل وملائكة النهار.
- قال ابن حجر: أن الصلاة في المسجد جماعة تزيد على الصلاة في البيت وفي السوق جماعة وفرادى، قاله ابن دقيق العيد.
- فيه فضيلة صلاة الفَجر؛ لاختصاص اجتماع الملائكة بها.
- قال ابن باز: ينبغي للمؤمن أن يحرص على المحافظة على الصلاة في جماعة ولو بَعُدت داره لينال هذا الخير العظيم.
- قال النووي في الجمع بين الروايات أن صلاة الجماعة تفضل صلاة الفذ بخمس وعشرين درجة، والأخرى بسبع وعشرين: والجمع بينهما من ثلاثة أوجه: أحدها: أنه لا منافاة فذِكْر القليل لا ينفي الكثير، ومفهوم العدد باطل عند الأصوليين، والثاني: أن يكون أخبر أولًا بالقليل ثم أعلمه الله تعالى بزيادة الفضل فأخبر بها، الثالث: أنه يختلف باختلاف أحوال المصلين والصلاة، وتكون لبعضهم خمس وعشرون، ولبعضهم سبع وعشرون بحسب كمال الصلاة ومحافظته على هيئاتها وخشوعها وكثرة جماعتها وفضلهم وشرف البقعة ونحو ذلك، والله أعلم.