Hadithi

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Matini ya Kiarabu

عن علي بن أبي طالب، ومعاذ بن جبل رضي الله عنهما مرفوعًا: «إذا أتى أحدُكم الصلاةَ والإمامُ على حال، فلْيصنعْ كما يصنع الإمامُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Ally bin Abii Twalib, na Mua'dh bin Jabali- radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Hadithi Marfu'u: "Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, basi na afanye kama anavyofanya imamu".

Ufafanuzi

Atakapokuja mmoja wenu katika swala na imamu akawa yuko katika hali fulani, ima ya kusimama au kurukuu au kusujudu au kukaa, basi aendane na imamu pale alipo katika kusimama au kurukuu au kitendo kinginecho, na asisubiri mpaka anyanyuke imamu kama wanavyofanya baadhi ya watu.

Mafunzo

  • Sheria ya kuingia mwenye kuungana pamoja na imamu katika kipengele chochote miongoni mwa vipengele vya swala atakachokikuta, bila kutofautisha kati ya rukuu na sijida na kukaa.
  • Nikuwa kuipata rakaa ambayo ameungana na imamu kunakuwa kwa kuikuta rukuu yake, kama zilivyoonyesha juu ya hilo dalili zingine.
Ufafanuzi: العربية

إذا أتى أحدكم الصلاة والإمام على حال من قيام أو ركوع أو سجود أو قعود، فليوافق الإمام فيما هو فيه من القيام أو الركوع أو غير ذلك، ولا ينتظر حتى يقوم الإمام كما يفعله العوام.

  • مشروعية دخول اللاحق مع الإمام في أي جزء من أجزاء الصلاة أدركه، من غير فرق بين الركوع والسجود والقعود.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi