Hadithi

Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أبي بكرة رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «‌أَلَا ‌أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ؟» ثَلَاثًا، قَالُوا: بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ» وَجَلَسَ وَكَانَ مُتَّكِئًا، فَقَالَ: «أَلَا وَقَوْلُ الزُّورِ»، قَالَ: فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا: لَيْتَهُ سَكَتَ.

Tafsiri

Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.

Ufafanuzi

Anawaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba zake kuhusu madhambi makubwa, akataja haya matatu: 1- Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu: Nako ni kuielekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiye Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika uungu wake na uumbaji na ulezi wake na majina yake na sifa zake. 2- Kuwaasi wazazi wawili: Nayo ni kila aina ya maudhi kwa wazazi wawili, sawa sawa iwe kwa kauli au kitendo, na kuacha kuwafanyia wema. 3- Kauli ya uongo ikiwemo ushahidi wa uongo: Nayo ni kila kauli ya kuzusha ya uongo, yenye lengo la kumdhalilisha yule anayekusudiwa kwa kuchukua mali yake au kumfanyia uadui katika heshima yake au mfano wa hayo. Alikariri Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari hii ya kusema uongo ikiwa ni tahadhari juu ya ubaya wake na athari zake mbaya kwa jamii, mpaka wakasema Masahaba: Laiti angelinyamaza; Kwa sababu ya kumhurumia, na kwa kuchukia kile kinachompa kero Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Mafunzo

  • Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu amelifanya kuwa dhambi kubwa la kwanza na kubwa kuliko yote, na inayotia mkazo katika hili ni kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi pale anaposhirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye".
  • Ukubwa wa haki ya wazazi wawili, pale alipoambatanisha haki zao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  • Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
Ufafanuzi: العربية

يُخبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أصحابَه عن أعظم الكبائر، فذَكرَ هذه الثلاث: 1. الإشراك بالله: وهو صَرْفُ أيِّ نوعٍ من أنواع العبادة لغير الله، وتسويةُ غيرِ الله بالله في ألوهيته وربوبيته وأسمائه وصفاته. 2. عقوق الوالدين: وهو كلُّ أذى للأبوين، قولًا كان أو فعلًا، وترك الإحسان إليهما. 3. قول الزور ومنه شهادة الزور: وهو كل قول مُزوَّر ومكذوب يراد به انتقاص مَن وقع عليه بأخذ ماله أو الاعتداء على عرضه أو نحو ذلك. وقد كَرَّر النبيُّ صلى الله عليه وسلم التحذيرَ من قول الزور تنبيهًا على استقباحِه وآثارِه السيئة على المجتمع، حتى قال الصحابة: ليته سكت؛ شَفقةً عليه، وكراهية لِما يُزعجه.

  • أعظم الذنوب الشركُ بالله؛ لأنه جعلَه صَدْرَ الكبائر وأكبرَها، ويؤكد هذا قوله تعالى {إن الله لا يَغْفِرُ أن يشرَكَ به وَيَغْفِرُ مَا دونَ ذلِكَ لِمَنْ يشَاء}.
  • عظم حقوق الوالدين، إذ قَرَنَ حقَّهما بحق الله تعالى.
  • الذنوب تنقسم إلى كبائر وصغائر، والكبيرة هي: كلُّ ذنب فيه عقوبة دنيوية، كالحدود واللعن، أو وعيد أُخروي، كالوعيد بدخول النار، وأن الكبائر دركات بعضها أغلظ من بعض في التحريم، وصغائر الذنوب هي ما سوى الكبائر.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi