Hadithi

Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ السَّاعِدِيِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «رِبَاطُ يَوْمٍ فِي سَبِيلِ اللَّهِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَمَوْضِعُ سَوْطِ أَحَدِكُمْ مِنَ الجَنَّةِ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا، وَالرَّوْحَةُ يَرُوحُهَا العَبْدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ أَوِ الغَدْوَةُ خَيْرٌ مِنَ الدُّنْيَا وَمَا عَلَيْهَا».

Tafsiri

Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad radhi za Allah ziwe juu yake hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Kudumu siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na sehemu ya mjeledi wa mmoja wenu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake, na kutoka asubuhi kwa mja katika njia ya Mwenyezi Mungu au kutoka mchana ni bora kuliko dunia na vilivyo juu yake".

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kubakia katika eneo ambalo liko kati ya waislamu na makafiri kwa ajili ya kuwalinda dhidi yao kwa siku moja, kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba mahali pa kuweka mjeledi unaotumika kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu peponi ni bora kuliko dunia na vilivyomo, na kwamba malipo na thawabu za kutembea katika wakati wa mwanzo wa mchana mpaka mwanzo wa wakati wa adhuhuri, au mchana: Ni kwanzia adhuhuri mpaka usiku katika njia ya Mwenyezi Mungu mara moja, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.

Mafunzo

  • Fadhila za kuthubutu katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya hatari zilizomo zinazoihatarisha nafsi, na kwa yale yanayofungamana nalo kama kulinyanyua neno la Mwenyezi Mungu na kuitetea dini yake, kwa hivyo, thawabu za siku moja pekee, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  • Udhalili wa dunia ukiilinganisha na akhera; kwa sababu sehemu ya kuweka mjeledi pekee peponi, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  • Ubora wa kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ukubwa wa thawabu zake; kwa sababu thawabu za mwendo mmoja wa asubuhi au mchana, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.
  • Kauli yake: "Katika njia ya Mwenyezi Mungu" hapa kuna dalili ya umuhimu wa kutakasa nia, na kwamba malipo yanaambatana na hilo.
Ufafanuzi: العربية

يخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن ملازمة المكان الذي بين المسلمين والكفار لحراسة المسلمين منهم ليوم واحد مُخلصًا لله خير من الدنيا وما فيها، وأن موضع السوط الذي يجاهد به في سبيل الله في الجنة خير من الدنيا وما فيها، وأن أجر وثواب السير في الوقت الذي من أول النهار إلى بداية وقت الظهر، أو الروحة: من وقت الظهر إلى الليل في سبيل الله مرة واحدة، خير من الدنيا وما فيها.

  • فضل الرباط في سبيل الله، لما فيه من المخاطرة بالنفس، ولما يترتب عليه من إعلاء كلمة الله ونصر دينه؛ لذا فإن ثواب يوم واحد، خير من الدنيا وما فيها.
  • حقارة الدنيا بالنسبة للآخرة؛ لأن موضع السوط من الجنة، خير من الدنيا وما فيها.
  • فضل الجهاد في سبيل الله، وعظم ثوابه؛ لأن ثواب الروحة الواحدة أو الغدوة، خير من الدنيا وما فيها.
  • قوله: "في سبيل الله" فيه الدلالة على أهمية الإخلاص، وأن الأجر مترتب عليه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi