Hadithi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ، فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهِ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akipenda na akipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yanayostahiki heshima, na miongoni mwake ni: Kuanza na mguu wa kulia katika kuvaa viatu vyake, na kuanzia kulia katika kutana nywele za kichwa chake, kuziachanisha kwake na kuzipaka kwake mafuta, na katika kutawadha kwake, anatanguliza kulia kabla ya kushoto katika mikono na miguu.

Mafunzo

  • Amesema Imam Nawawi: Hii ni kanuni endelevu katika Sheria, kuwa kila jambo la heshima na utukufu kama vile kuvaa nguo, suruali, kandambili, kuingia msikitini, kupiga mswaki, kupaka wanja, kukata kucha, kupunguza masharubu, kuchana nywele, kung'oa nywele za kwapa, kunyoa kichwa, kutoa salam ya kumaliza swala, na kuosha viungo kwa ajili ya usafi, na kutoka nje ya choo, kula na kunywa, kupeana mikono, kugusa Jiwe Jeusi, na mambo mengine yenye kufanana na haya, basi ni sunna kuanza na upande wa kulia, na ama yale yaliyo kinyume chake, kama vile kuingia chooni, kutoka msikitini, kukidhi haja ndogo, kujisafisha, kuvua nguo, suruali, kandambili, na kadhalika, haya ni sunna kuanza na upande wa kushoto, na yote hayo ni kwa sababu ya heshima ya upande wa kulia na utukufu wake.
  • "Anapendezwa na kuanzia kulia" Inajumuisha: Kuanza vitendo kwa mkono wa kulia, mguu wa kulia, upande wa kulia, na kushughulikia kitu kwa mkono wa kulia.
  • Amesema Imam Nawawi: Tambueni kuwa miongoni mwa sehemu za udhu kuna ambazo hazipendezi kuanzia kulia; ambazo ni masikio, viganja, na mashavu, bali vitasafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa halitowezekana hilo kama ilivyo kwa mtu aliyekatwa sikio na mfano wake; basi atatanguliza upande wa kulia.
Ufafanuzi: العربية

كانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم يحبُّ ويفضِّل أن يبدأ باليمين في أموره اللائقة بالتكريم، ومن ذلك: أن يبدأ بالرِّجْل اليمين في لبس نعله، ويبدأ باليمين في ترجيل شعر رأسه ولحيته وتسريحِهما ودَهنِهما، وفي وضوئه يقدِّم اليمين على اليسار من اليدين والرجلين.

  • قال النووي: هذه قاعدة مستمرة في الشرع، وهي أنَّ ما كان من باب التكريم والتشريف كلبس الثوب والسراويل والخُفِّ ودُخول المسجد والسواك والاكتحال، وتقليم الأظفار، وقص الشارب، وتَرْجِيْل الشَّعَرِ وهو مَشْطُه، ونتف الإبط، وحلق الرأس، والسلام من الصلاة، وغسل أعضاء الطهارة، والخروج من الخلاء، والأكل والشرب، والمصافحة، واستلام الحجر الأسود، وغير ذلك مما هو في معناه يستحب التيامن فيه، وأما ما كان بضده كدخول الخلاء والخروج من المسجد والامتخاط والاستنجاء وخلع الثوب والسراويل والخف وما أشبه ذلك، فيستحب التياسر فيه، وذلك كله بكرامة اليمين وشرفها.
  • "يعجبه التيمن"، يشمل: الابتداء في الأفعال باليد اليمنى، والرجل اليمنى، والجانب الأيمن، وتعاطي الشيء باليمين.
  • قال النووي: اعلم أن من أعضاء الوضوء ما لا يستحب فيه التيامن؛ وهو الأذنان والكفان والخدان بل يُطَهَّران دفعة واحدة، فإن تعذَّر ذلك كما في حق الأقطع ونحوه؛ قَدَّمَ اليمين.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi