Hadithi

hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ أَبِي حُبَيْشٍ سَأَلَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَتْ: إِنِّي أُسْتَحَاضُ فَلاَ أَطْهُرُ، أَفَأَدَعُ الصَّلاَةَ؟ فَقَالَ: «لَا، إِنَّ ذَلِكِ عِرْقٌ، وَلَكِنْ دَعِي الصَّلاَةَ قَدْرَ الأَيَّامِ الَّتِي كُنْتِ تَحِيضِينَ فِيهَا، ثُمَّ اغْتَسِلِي وَصَلِّي».

Tafsiri

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Mimi hupatwa na hedhi ya ugonjwa na sitwahariki, je niache swala? Akasema: "Hapana, hakika hilonitatizolinatokananamshipawakizazikukatika, lakini acha swala kwa kiasi cha siku ulizokuwa ukipata hedhi ndani yake, kisha oga na swali".

Ufafanuzi

Fatma bint Abii Qubaishi alimuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi damu haikatiki kwangu na huendelea hata nje ya wakati wa hedhi, je itakuwa hukumu ya damu hiyo ni hukumu ya damu ya hedhi ili niache swala? Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema kumwambia: Hiyo ni damu ya ugonjwa, nayo ni damu ya ugonjwa ambayo husababishwa na kukatika kwa mshipa katika mfuko wa uzazi, na si damu ya hedhi, Unapokuja muda wa hedhi uliokuwa ukipata hedhi ndani yake kwa mujibu wa ada yako ya mwezi kabla hujaugua, basi acha swala na swaumu na mengineyo anayozuiliwa kuyafanya mwenye hedhi wakati wa hedhi. Kinapomalizika kiwango cha muda huo, hapo utakuwa umetwaharika na hedhi, osha mahali palipo na damu, kisha osha mwili wako josho kamili kwa ajili ya kuondoa hadathi, kisha swali.

Mafunzo

  • Uwajibu wa kuoga kwa mwanamke zinapomalizika siku za hedhi yake.
  • Uwajibu wa kuswali kwa mwenye istihadha (Hedhi ya ugonjwa).
  • Hedhi: Ni damu ya maumbile ambayo hutolewa na mfuko wa uzazi kupitia tupu ya mwanamke aliyevunja ungo, humpata katika siku maalum.
  • Istihadha: Ni kutiririka kwa damu nje ya wakati wake kutoka nje ya mfuko wa uzazi na si ndani yake.
  • Tofauti kati ya istihadha na damu ya hedhi: Nikuwa damu ya hedhi ni nyeusi nzito inaharufu mbaya, ama damu ya istihadha ni nyekundu nyepesi na haina harufu mbaya.
Ufafanuzi: العربية

سَألتْ فاطمةُ بنت حبيش النبيَّ صلى الله عليه وسلم فقالت: إني لا ينقطع عني الدم ويستمر حتى في غير زمن الحيض، فهل يكون حكم ذلك حكم الحيض فأترك الصلاة؟ فقال لها النبي صلى الله عليه وسلم: إنه دم استحاضة، وهو دم مَرَضِيٌّ ينشأ عن انقطاع عرق في الرحم، وليس بدم حيض، فإذا جاء وقت الحيض الذي كنت تحيضين فيه على عادتك الشهرية قبل أن تمرضين بالاستحاضة، فاتركي الصلاة والصوم وغيرَهما مما تُمنَع منه الحائض وقت الحيض. فإذا انتهى مقدار تلك المدة، فتكوني قد طهرتي من الحيض، فاغسلي موضع الدم، ثم اغسلي بدنك اغتسالًا كاملًا لرفع الحدث، ثم صلي.

  • وجوب الغسل على المرأة عند انتهاء أيام حيضها.
  • وجوب الصلاة على المستحاضة.
  • الحيض: دمُ طبيعةٍ يُرْخِيْه الرَّحِمُ عَبْرَ فَرْجِ المرأةِ البالغة، يصيبها في أيام معلومة.
  • الاستحاضة: سَيَلانُ الدمِ في غير وقته من أدنى الرحم دون قَعْرِه.
  • الفرق بين دم الحيض ودم الاستحاضة: أنَّ دمَ الحيضِ أسود ثخين مُنْتِن الرائحة، أما دم الاستحاضة فأحمر رقيق ليس له رائحة منتنة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi