Hadithi

Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي لله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً، إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ» أَوْ قَالَ: «غَيْرَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.

Mafunzo

  • Huu ni wito kwa muumini wa kuja katika haki na uadilifu, na kuhukumu mambo kwa akili katika mgogoro wowote unaotokea baina yake na mke wake, na sio kutoa maamuzi kwa hisia na mihemuko ya muda mfupi.
  • Kazi ya muumini si kumchukia mwanamke muumini kabisa mpaka afikie kuachana naye, bali apuuze kile anachochukia kwa kile anachopenda.
  • Himizo la kuishi vizuri na kutengeneza urafiki kati ya wanandoa.
  • Imani ni msukumo wa maadili mema, hivyo hakuna muumini wa kiume au wa kike asiye na tabia njema; Imani inachochea uwepo wa sifa njema ndani yao.
Ufafanuzi: العربية

نَهَى النبيُّ صلى الله عليه وسلم الزوج أن يُبغض زوجتَه بُغضًا يؤدّي إلى ظلمها وتركها والإعراض عنها؛ فإن الإنسان مجبول على النقص، وإن كره منها خُلقًا سيئًا، وجد فيها خلقًا آخر حسنًا؛ فيرضى بالحَسَن الذي يوافقه، ويصبر على ما لا يرضى من السيئ، مما يجعله يصبر ولا يكرهها كرهًا يحمله على فراقها.

  • دعوة المؤمن إلى العدل وتحكيم العقل في أي خلاف ينشأ مع زوجته، وعدم اللجوء إلى تحكيم العاطفة والانفعالات المؤقتة.
  • شأن المؤمن أن لا يبغض المؤمنة بغضًا كليًّا يحمله على فراقها، بل الذي ينبغي عليه أن يتغاضى عما يكره بما يحب.
  • الحث على حسن العشرة والصحبة بين الزوجين.
  • الإيمان داع لمكارم الأخلاق، فلا يخلو المؤمن والمؤمنة من خلق حسن؛ فالإيمان يستلزم وجود خصال محمودة فيهما.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi