Hadithi

Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّهُ لَقِيَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ وَهُوَ جُنُبٌ، فَانْسَلَّ فَذَهَبَ فَاغْتَسَلَ، فَتَفَقَّدَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا جَاءَهُ قَالَ: «أَيْنَ كُنْتَ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ؟» قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، لَقِيتَنِي وَأَنَا جُنُبٌ فَكَرِهْتُ أَنْ أُجَالِسَكَ حَتَّى أَغْتَسِلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سُبْحَانَ اللهِ، إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَا يَنْجُسُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".

Ufafanuzi

Alikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.

Mafunzo

  • Janaba linamzuia mtu kuswali na kugusa msahafu na kukaa msikitini, na wala halizuii kukaa pamoja na Waislamu na kukutana nao, na wala mwenye janaba hawi najisi.
  • Usafi wa muumini akiwa hai au maiti.
  • Kuwaheshimu watu wenye heshima, na elimu, na utengefu, na kukaa nao kwa muonekano mzuri.
  • Hapa kuna sheria ya mfuasi kumuomba idhini ya kuondoka anayemfuata, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimkemea Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa kuondoka kwake pasina yeye kujua, na hii ni kwa sababu kuomba ruhusa ni katika adabu nzuri.
  • Kusema: Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, wakati wa kustaajabu.
  • Kufaa mtu kusimulia mambo yake binafsi katika yale ya aibu, kwa ajili ya masilahi.
  • Kafiri ni najisi, lakini najisi yake si ya kuonekana, kwa sababu ya uchafu wa itikadi yake.
  • Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii pia kuna adabu, ya kwamba msomi atakapoona kwa anayemfuata jambo analohofia kwake kwenda kinyume na usahihi basi amuulize, na amwambie lililo sahihi, na ambainishie hukumu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Ufafanuzi: العربية

لقي النبيُّ صلى الله عليه وسلم أبا هريرة رضي الله عنه في بعض طرق المدينة، وكان أبو هريرة على جنابة، ومن تعظيمه للنبي صلى الله عليه وسلم كره مجالسته ومحادثته وهو على تلك الحال ظنًّا منه أنه نجس، فذهب في خُفية واغتسل، ثم رجع وجلس، فسأله النبي صلى الله عليه وسلم أين ذهب؟ فأخبره بحاله، وأنه كره مجالسته وهو نجس من الجنابة، فتعجب النبي صلى الله عليه وسلم وقال له: إن المؤمن طاهر ولا ينجس على كل حال؛ حيًّا ولا ميتًا.

  • الجنابة إنما تمنع من الصلاة ومس المصحف والمكوث في المسجد، ولا تمنع من مجالسة المسلمين ومقابلتهم، ولا يصير بها الجنب نجسًا.
  • طهارة المؤمن حيًّا وميتًا.
  • تعظيم أهل الفضل، والعلم، والصلاح، ومجالستهم على أحسن الهيئات.
  • مشروعية استئذان التابع للمتبوع في الانصراف، فقد أنكر النبي صلى الله عليه وسلم على أبي هريرة رضي الله عنه، ذهابه من غير علمه، وذلك أن الاستئذان من حسن الأدب.
  • قول: سبحان الله، عند التعجب.
  • جواز تحدث الإنسان عن نفسه بما يُستحيا منه للمصلحة.
  • الكافر نجس، لكن نجاسته معنوية لخبث عقيدته.
  • قال النووي: وفي هذا الحديث أيضًا من الآداب أن العالم إذا رأى من تابعه أمرًا يخاف عليه فيه خلاف الصواب سأله عنه، وقال له صوابه، وبين له حكمه، والله أعلم. ‏

Mada

Ripoti kosa

Zaidi