Hadithi

Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «أَمَا يَخْشَى أَحَدُكُمْ - أَوْ: لاَ يَخْشَى أَحَدُكُمْ - إِذَا رَفَعَ رَأْسَهُ قَبْلَ الإِمَامِ، أَنْ يَجْعَلَ اللَّهُ رَأْسَهُ رَأْسَ حِمَارٍ، أَوْ يَجْعَلَ اللَّهُ صُورَتَهُ صُورَةَ حِمَارٍ».

Tafsiri

Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hivi haogopi mmoja wenu (Au: Hachelei mmoja wenu) atakapoinua kichwa chake kabla ya imamu, Mwenyezi Mungu akifanye kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye Mwenyezi Mungu sura yake kuwa sura ya punda".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ahadi ya adhabu kali kwa mwenye kunyanyua kichwa chake kabla ya imamu wake, kuwa Mwenyezi Mungu kukifanya kichwa chake kuwa kichwa cha punda, au aifanye sura yake kuwa sura ya punda.

Mafunzo

  • Maamuma anapokuwa na imam kuna hali nne: haliTatu zimekatazwa, nazo ni: Kumtangulia, na kwenda naye sawa, na kuchelewa, na mafundisho kwa maamuma: Ni kumfuata imam.
  • Ulazima wa maamuma kumfuata imam ndani ya swala.
  • Ahadi ya adhabu ya kubadilika sura kwa atakayenyanyua kichwa chake kabla ya imam na kuwa sura ya punda ni jambo linawezekana, nako ni kufutwa kwa sura halisi.
Ufafanuzi: العربية

يُبَيِّنُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم الوعيدَ الشديدَ على مَن يَرفَعُ رأسَه قبل إمامِهِ، بأنْ يجعلَ اللهُ رأسَه رأسَ حِمار، أو يَجعلَ صورتَه صورةَ حمار.

  • للمأموم مع الإمام أربع حالات: ثلاث منهي عنها، وهي: المسابقة والموافقة والتأخر، والمشروع للمأموم: المتابعة للإمام.
  • وجوب متابعة المأموم للإمام في الصلاة.
  • الوعيدُ بتغيير صورة من يرفع رأسه قبل الإمام إلى صورة حمار أَمْرٌ ممكن، وهو مِن المسخ.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi