Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ السَّاعَةِ، فَقَالَ: مَتَى السَّاعَةُ؟ قَالَ: «وَمَاذَا أَعْدَدْتَ لَهَا». قَالَ: لاَ شَيْءَ، إِلَّا أَنِّي أُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ». قَالَ أَنَسٌ: فَمَا فَرِحْنَا بِشَيْءٍ، فَرِحْنَا بِقَوْلِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَنْتَ مَعَ مَنْ أَحْبَبْتَ» قَالَ أَنَسٌ: فَأَنَا أُحِبُّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَبَا بَكْرٍ، وَعُمَرَ، وَأَرْجُو أَنْ أَكُونَ مَعَهُمْ بِحُبِّي إِيَّاهُمْ، وَإِنْ لَمْ أَعْمَلْ بِمِثْلِ أَعْمَالِهِمْ.
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake-: Yakuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu Kiyama, akasema: Lini Kiyama? Akasema: “Umetayarisha nini kwa ajili yake?” Akasema: Hapana, isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake. Akasema: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Hakuna lililotufurahisha zaidi ya kauli ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake: “Wewe uko pamoja na unayempenda.” Anas akasema: Mimi ninampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na ninataraji kuwa pamoja nao kutokana na mapenzi yangu kwao, hata kama nisipofanya sawa na matendo yao.
Ufafanuzi
Bedui mmoja anayeishi jangwani alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Je, saa ya Kiyama itatokea wakati gani? Basi rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Umeiandalia mambo gani mema? Akasema muulizaji: Sikutayarisha jambo kubwa kwa ajili yake isipokuwa ninampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wala hakutaja ibada nyinginezo za moyo, za kimwili, au za kifedha. Kwa sababu zote ni matawi ya upendo unaotokana na hayo, na kwa sababu upendo wa dhati humsukuma mtu kujitahidi kufanya matendo mema. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Wewe utakuwa pamoja na unayempenda peponi. Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakafurahishwa sana na habari hii njema. Kisha Anas radhi za Allah ziwe juu yake akaeleza kuwa hakika anampenda Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abubakari na Omari, na anatarajia kuwa pamoja nao, hata kama amali zake si kama amali zao.
Mafunzo
- Hekima ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kumjibu muulizaji, kwani alimuongoza katika yale yanayomhusu na kumuokoa, nayo ni: kujiandaa na Akhera kwa yenye manufaa na matendo mema.
- Mwenyezi Mungu ameficha kwa waja wake elimu ya kujua Kiyama, ili mtu aendelee kuwa tayari na kujiandaa kukutana na Mwenyezi Mungu.
- Fadhila za kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na watu wema miongoni mwa waumini, na onyo la kuwapenda washirikina.
- Kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Wewe utakuwa pamoja na umpendaye. Kinachokusudiwa sio usawa wa daraja na hadhi, bali ni kuwa, wao watakuwa Peponi kiasi kwamba kila mmoja wao ataweza kumuona mwenzake, hata kama sehemu hiyo iko mbali.
- Kumuelekeza Muislamu kuzingatia yale yaliyo bora na yenye manufaa kwake, na kuacha kuuliza juu ya yale ambayo hayamnufaishi.
Ufafanuzi: العربية
سَألَ النبيَّ صلى الله عليه وسلم رجلٌ أعرابيٌّ مِمّن يَسكن الصحراء: عن وقت قيام الساعة؟ فقال له صلى الله عليه وسلم: وما أعددتَ لها من العمل الصالح؟ فقال السائل: ما أعددتُ لها كبيرَ عملٍ إلا أني أحبُّ اللهَ ورسولَه، ولم يذكر غيرَها من العبادات القلبية والبدنية والمالية؛ لأنها كلُّها فروع للمحبة مترتبة عليها، ولأن المحبة الصادقة باعثة للاجتهاد في العمل الصالح. فقال له صلى الله عليه وسلم: إنك مع مَن أحببتَ في الجنة. ففرح أصحابُ النبيِّ صلى الله عليه وسلم بهذه البشرى فرحًا شديدًا. ثم أَخبرَ أنسٌ رضي الله عنه أنه يحب النبي صلى الله عليه وسلم وأبا بكر، وعمر، ويرجو أن يكون معهم، وإن كان عملُه ليس مثلَ عملِهم.
- حكمة رسول الله صلى الله عليه وسلم في إجابة السائل، حيث دلَّه على الذي يهمه وينجيه، وهو: الاستعداد للآخرة بما ينفع والعمل الصالح.
- أخفى اللهُ علمَ الساعة على العباد ليبقى المرء مستعدًّا متجهزًا للقاء الله.
- فضل محبة الله ورسوله والصالحين من المؤمنين، والتحذير من محبة المشركين.
- قوله صلى الله عليه وسلم: أنت مع من أحببت. ليس المراد التساوي في الدرجة والمنزلة، بل المراد كونهم في الجنة بحيث يتمكَّن كل واحد منهم من رؤية الآخر وإن بَعُد المكان.
- توجيه المسلم للانشغال بالأصلح والأنفع له، وترك السؤال عما لا ينفعه.