Hadithi

Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن أبِي هريرة رضي اللَّه عنه: سمعتُ النبِيّ صلى الله عليه وسلم يقول: «الفِطْرَةُ خمسٌ: الخِتَانُ والاستحدادُ وقصُّ الشَّارِبِ وتقليمُ الأظفارِ وَنَتْفُ الآبَاطِ».

Tafsiri

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairi, na kunyoa sehemu za siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha na kunyofoa nywele za kwapa".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo matano katika dini ya Uislamu na sunna ya Mitume: La kwanza: Kutairi, nako ni kukata ngozi iliyozidi juu ya kichwa cha dhakari kwa mwanaume, na kukata kingozi katika tupu ya mwanamke juu ya malaha palipo tundu la uke. La pili: Kunyoa sehemu za siri, nako ni kunyoa nywele za kinena zinazozunguka tupu ya mbele. La tatu: Kupunguza masharubu, nako ni kupunguza kilichoota juu ya mdomo wa juu wa mwanaume mpaka mdomo uonekane wazi. La nne: Kupunguza kucha. La tano: Kunyofoa nywele za kwapa.

Mafunzo

  • Sunna za Mitume anazozipenda Mwenyezi Mungu na kuziridhia na anaziamrisha, zinapelekea katika ukamilifu na usafi na uzuri.
  • Sheria ya kushikamana na mambo haya, na kutoghafilika nayo.
  • Mambo haya yanafaida za kidini na kidunia, miongoni mwake: Kupendezesha muonekanao, na kusafisha mwili, na kujiweka tayari kwa usafi, na kwenda kinyume na makafiri, na kutekeleza amri ya Allah.
  • Kumetajwa katika hadithi zingine ziada ya jambo jingine la kimaumbile tofauti na matano haya, mfano: Kufuga ndevu, na mswaki na nyinginezo.
Ufafanuzi: العربية

بَيَّنَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم خمسَ خصالٍ من دينِ الإسلام وسنن المرسلين: أولها: الختان، وهو قطع جِلْدَةٍ زائدةٍ على الذَّكَرِ فوق الحَشَفَة، وقطعُ رأسِ جِلدةٍ في فرج الأنثى فوق مَحَلِّ الإيلاج. وثانيها: الاستحداد، وهو حَلْقُ شَعَرِ العَانَة الذي حول القُبُل. وثالثها: قص الشارب، وهو قصُّ ما نبت على شفة الرجل العليا بحيث تظهر الشفة. ورابعها: قص الأظفار. وخامسها: نتف الإبط.

  • سُنَنُ المرسلين التي يُحِبُّها الله ويرتضيها ويأمر بها تدعو إلى الكمال والنزاهة والجمال.
  • مشروعية تَعَاهُدِ هذه الأشياء، وعدم الغفلة عنها.
  • لهذه الخصال فوائد دينية ودنيوية، منها: تحسين الهيئة، وتنظيف البدن، والاحتياط للطهارة، ومخالفة الكفار، وامتثال أمر الله.
  • ذُكِرَ في أحاديث أخرى زيادةُ خصالٍ للفطرةِ غيرِ هذه الخمس، مثل: إعفاء اللحية، والسواك، وغيرها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi