Hadithi

, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُبَادَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ، وَالْجَنَّةُ حَقٌّ، وَالنَّارُ حَقٌّ، أَدْخَلَهُ اللهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنَ الْعَمَلِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Ubada bin -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayetamka neno la tauhidi kwa kujua maana yake, kwa kuyafanyia kazi madhumuni yake, na akashuhudia utumwa wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- na ujumbe wake, na akakiri utumwa wa Issa na ujumbe wake, Na kuwa Mwenyezi Mungu alimuumba kwa kauli yake "Kuwa" na akawa, na kuwa yeye ni roho miongoni mwa roho alizoziumba Mwenyezi Mungu, Na akamtenga mbali mama yake kwa yale waliyomnasibisha nayo Mayahudi, Nakuwa atakayeamini pepo kuwa ni kweli, na kuwa Moto ni kweli, akaitakidi uwepo wake, nakuwa hizo ni neema za Mwenyezi Mungu na adhabu yake, Na atakayekufa katika imani hiyo; basi mafikio yake ni Peponi hata kama alikuwa mzembe katika ibada, na anamadhambi.

Mafunzo

  • Mwenyezi Mungu Mtukufu kamuumba Issa mwana wa Mariamu kwa neno (Kuwa) bila baba.
  • Kinachowakusanya pamoja kati ya Issa (Yesu) na Muhammadi amani iwe juu yao wote ni kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, basi wao wote wawili ni Mitume hawasemi uongo, na ni waja wala hawaabudiwi.
  • Ubora wa tauhidi na kufuta kwake madhambi, nakuwa mafikio ya mtu wa tauhidi ni Peponi, hata kama yakajitokeza kwake baadhi ya madhambi.
Ufafanuzi: العربية

يُخْبِرُنا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم أنَّ مَن نَطَقَ بكلمةِ التوحيد عارفًا لمعناها عاملًا بمقتضاها، وشهد بعبودية محمد صلى الله عليه وسلم ورسالته، واعترف بعبودية عيسى ورسالته، وأنَّ الله خلقه بقوله "كن" فكان، وأنه روح من الأرواح التي خلقها الله، وَبَرَّأَ أُمَّهُ مِمّا نَسَبَه إليها اليهود، وآمن بأن الجنة حق، وأن النار حق، معتقدًا وجودهما، وأنهما نعيم الله وعذابه، ومات على ذلك؛ فمصيره إلى الجنة وإن كان مقصِّرًا في الطاعات، وله ذنوب.

  • الله تعالى خَلَقَ عيسى ابن مريم بكلمة (كُنْ) من غير أب.
  • الجمع بين كون عيسى ومحمد صلى الله عليهما وسلم عبدي الله ورسوليه، فهما رسولان لا يكذبان، وعبدان لا يُعْبَدان.
  • فضل التوحيد وتكفيره للذنوب، وأنَّ مصيرَ الموحِّد الجنةُ وإنْ وقع منه بعض الذنوب.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi