Hadithi

Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أُمِّ قَيْسٍ بِنْتِ مِحْصَنٍ رَضيَ اللهُ عنها: أَنَّهَا أَتَتْ بِابْنٍ لَهَا صَغِيرٍ لَمْ يَأْكُلِ الطَّعَامَ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَجْلَسَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي حَجْرِهِ، فَبَالَ عَلَى ثَوْبِهِ، فَدَعَا بِمَاءٍ، فَنَضَحَهُ وَلَمْ يَغْسِلْهُ.

Tafsiri

Kutoka kwa Ummu Qais bint Mihswan -radhi za Allah ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake mdogo hajaanza kula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, akakojoa katika nguo yake, akaomba maji, akanyunyizia na wala hakuosha.

Ufafanuzi

Alikuja mama Kaisi binti Mihswan radhi za Allah ziwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa na mtoto wake hajaanza kula chakula kutokana na udogo wa umri wake, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamkalisha katika mapaja yake, mtoto akakojoa katika nguo yake rehema na amani ziwe juu yake, akaomba maji, na akanyunyiza katika nguo yake na wala hakuiosha.

Mafunzo

  • Tabia njema za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na unyenyekevu wake wa hali ya juu.
  • Wito wa kuishi vizuri na watu na unyenyekevu na upole kwa watoto, na kulea nyoyo za watu wazima kwa kuwakirimu watoto wao na kuwakalisha mapajani, na mfano wa hayo.
  • Najisi ya mkojo wa mtoto mdogo hata asipokula chakula kwa matamanio.
  • Kitendo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kinaitwa kunyunyiza, hicho ni maalumu kwa mtoto mdogo wa kiume ambaye hajaanza kula chakula, ama mtoto wa kike ni lazima kuosha mkojo wake hata akiwa mdogo.
  • Kinyesi cha mtoto wa kiume ambaye chakula chake ni maziwa ya mama yake ni lazima kuosha kama najisi zingine.
  • Kuosha ni lazima kuwe na jambo la ziada kama kufikisha maji.
  • Kilicho bora ni kufanya haraka kusafisha mahali palipo na najisi; ili kufanya haraka kujitwaharisha kutokana na uchafu; na ili asisahau.
Ufafanuzi: العربية

أتتْ أمُّ قيس بنت محصن رضي الله عنها إلى النبي صلى الله عليه وسلم بابن لها لم يبدأ بأكل الطعام من صغر سنه، فأجلسه صلى الله عليه وسلم في حجره، فبال الصبي على ثوبه صلى الله عليه وسلم، فطلب ماء، ورشه على ثوبه ولم يغسله.

  • أخلاق النبي صلى الله عليه وسلم الكريمة، وتواضعه الجم.
  • الندب إلى حسن المعاشرة والتواضع والرفق بالصغار، وجبر قلوب الكبار بإكرام أطفالهم وإجلاسهم في الحجر، ونحو ذلك.
  • نجاسة بول الغلام وإن لم يأكل الطعام لشهوة.
  • فعل النبي صلى الله عليه وسلم يسمى نَضْحًا، وهو خاص بالطفل الصغير الذكر الذي لم يبدأ بأكل الطعام، أما الأنثى فلا بد من غسل بولها حتى ولو كانت صغيرة.
  • عَذِرَةُ الغلام الذي يتقوَّت من لبن أمه لا بُدَّ فيها من الغسل كسائر النجاسات.
  • الغسل لا بد فيه من أمر زائد على إيصال الماء.
  • الأولى المبادرة بتطهير محل النجاسة؛ للمسارعة في التطهر من الخبث؛ ولئلَّا ينسى.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi