Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الدُّنْيَا سِجْنُ الْمُؤْمِنِ وَجَنَّةُ الْكَافِرِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema: Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Dunia ni Gereza la Muumini na ni Pepo ya Kafiri".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba maisha ya Dunia kwa muumini ni kama Gereza analoishi kwa amri za kisheria, kama kufanya maamrisho na kuacha makatazo, basi akifa anapumzika na haya na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake, katika neema za kudumu, nayo kwa Kafiri ni kama Pepo; kwa sababu anafanya ndani yake kila inachotamani nafsi yake na kuamrishwa na matamanio yake, basi akifa anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya Kiyama miongoni mwa adhabu za kudumu.
Mafunzo
- Amesema Nawawi: Kila muumini ni mfungwa, amezuiliwa katika dunia kuyaendea matamanio yaliyoharamishwa pamoja na machukizo, amelazimishwa kufanya matendo ya utiifu na magumu, basi akifa anapumzika na haya, na anahamia katika yale aliyomuandalia Mwenyezi Mungu kwake miongoni mwa neema za kudumu, na raha halisi isiyokuwa na mapungufu, na ama Kafiri basi yeye huyamiliki hayo aliyoyapata katika starehe za dunia, pamoja nakuwa ni machache, na yamejawa tabu ziilizojaa vikwazo mbali mbali, hivyo, anapokufa anaingia katika adhabu ya kudumu, na mateso ya milele.
- Amesema Assanadi: Kauli yake: "Gereza la Muumini" Bila shaka hata kama ndani yake kuna neema, basi Pepo ni bora kwake kuliko hizo, "Na Pepo ya Kafiri" Basi hata kama kuna machukizo ila Moto ndio shari zaidi kwake kuliko hayo.
- Udhalili wa Dunia kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Dunia ni nyumba ya majaribu na mitihani kwa wenye imani.
- Kafiri ameiwahisha Pepo yake Duniani; akaadhibiwa kwa kunyimwa Pepo Akhera na neema zake.
Ufafanuzi: العربية
أخبر النبي صلى الله عليه وسلم أن الحياة الدنيا للمؤمن كالسجن لالتزامه بالتكاليف الشرعية من فعل المأمور وترك المحذور، فإذا مات استراح من هذا وانقلب إلى ما أعد الله تعالى له من النعيم الدائم، وهي للكافر كالجنة؛ لأنه يفعل فيها كل ما تشتهيه نفسه ويأمره به هواه، فإذا مات انقلب إلى ما أعد الله تعالى له يوم القيامة من العذاب المقيم.
- قال النووي: كل مؤمن مسجون ممنوع في الدنيا من الشهوات المحرمة والمكروهة، مكلف بفعل الطاعات الشاقة، فإذا مات استراح من هذا، وانقلب إلى ما أعد الله تعالى له من النعيم الدائم، والراحة الخالصة من النقصان، وأما الكافر فإنما له من ذلك ما حصل في الدنيا مع قلته وتكديره بالمنغصات، فإذا مات صار إلى العذاب الدائم، وشقاء الأبد.
- قال السندي: قوله (سجن المؤمن) فإنه وإن كان في نعمة فالجنة خير له منها، (وجنة الكافر) فإنه وإن كان في مقيتة فالنار شر له منها.
- هوان الدنيا على الله تعالى.
- الدنيا دار ابتلاء وامتحان لأهل الإيمان.
- الكافر استعجل جنته في دنياه؛ فعوقب بحرمان جنة الآخرة ونعيمها.