Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «السِّوَاكُ مَطْهَرَةٌ لِلْفَمِ، مَرْضَاةٌ لِلرَّبِّ».
Tafsiri
Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Mswaki ni usafi wa kinywa, humridhisha Mola".
Ufafanuzi
Anatueleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kusafisha meno kwa kijiti cha mti wa Arak na mfano wake husafisha kinywa kutokana na uchafu na harufu mbaya, Nakuwa ni katika sababu za kumridhisha Allah Mtukufu kwa mja; kwa sababu ndani yake kuna kumtii Allah na kuitika amri yake, na pia kuna usafi anaoupenda Allah Mtukufu.
Mafunzo
- Ubora wa mswaki, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuuhimiza umma wake kukithirisha kupiga
- Katika mswaki ni bora kutumia kijiti cha mti wa Arak, na kutumia miswaki ya brashi na dawa ya meno hukaa badala yake.
Ufafanuzi: العربية
يُخبرنا النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ تنظيفَ الأسنانِ بِعُوْدِ شجرةِ الأَرَاك ونحوِه يُطَهِّر الفَمَ من الأوساخ والروائح الكريهة، وأنه مِن أسباب رضا الله عن العبد؛ لأن فيه طاعة لله واستجابة لأمره، ولما فيه من النظافة التي يحبها الله تعالى.
- فضيلة التَّسَوُّك، وترغيب النبي صلى الله عليه وسلم أمَّته الإكثار منه.
- الأفضل في التسوُّك استعمال عُوْد شجر الأراك، واستعمل الفرشاة والمعجون يقومُ مقامَه.