Hadithi

Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، وَذَكَرَ الصَّدَقَةَ، وَالتَّعَفُّفَ، وَالمَسْأَلَةَ: «اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى، فَاليَدُ العُلْيَا: هِيَ المُنْفِقَةُ، وَالسُّفْلَى: هِيَ السَّائِلَةُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema huku akiwa juu ya Mimbari, na akataja sadaka, na kujizuia kuomba, na kuombaomba: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, mkono wa juu: Ni ule unaotoa, na mkono wa chini: Ni ule unaoomba".

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.

Mafunzo

  • Hapa kuna fadhila za ukarimu na utoaji katika njia za kheri, na ubaya wa kuombaomba.
  • Hapa kuna himizo la kujizuia kuomba, na kuwaepuka watu, na himizo la kufanya mambo matukufu, na kuacha yenye udhalili, na Mwenyezi Mungu anapenda mambo ya juu zaidi.
  • Mikono ina aina nne katika ubora, kama ifuatavyo: Wa juu zaidi ni ule unaotoa, kisha unaojizuia kuchukua, kisha unaopokea pasina kuomba, kisha unafuata wa chini kuliko hiyo, ule unaoomba.
Ufafanuzi: العربية

ذكر النبي صلى الله عليه وسلم وهو يخطب على المنبر الصدقة، والتعفف عن المسألة؛ ثم قال: اليد العليا المنفقة المعطية خير وأحب إلى الله من اليد السفلى السائلة.

  • فيه فضل البذل والإنفاق في وجوه الخير وذَمِّ السؤال.
  • فيه الحث على الاستعفاف عن المسألة والاستغناء عن الناس، والحض على معالي الأمور، وترك دَنِيئها، والله يحب معالي الأمور.
  • الأيدي أربع هي في الفضل كما يلي: أعلاها المنفقة، ثم المتعففة عن الأخذ، ثم الآخذة بغير سؤال، ثم وهي أدناها السائلة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi