Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه قَالَ: قُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ مَا النَّجَاةُ؟ قَالَ: «امْلِكْ عَلَيْكَ لِسَانَكَ، وَلْيَسَعْكَ بَيْتُكَ، وَابْكِ عَلَى خَطِيئَتِكَ».
Tafsiri
Kutoka kwa Ukba bin Aamir Al-Juhaniy -radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Ufafanuzi
Ukba bin Aamiri alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu sababu za muumini kuokoka katika dunia na Akhera? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Shikamana na mambo matatu: La kwanza: Hifadhi ulimi wako katika yale yasiyokuwa na kheri ndani yake, na kuzungumza kila shari, na usitamke ila la kheri. La pili: Baki nyumbani kwako ili umuabudu Mwenyezi Mungu katika nyakati za faragha, na ujishughulishe na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ibada, na jitenge nyumbani kwako na fitina. La tatu: Lia na ujute na utubie kwa yale uliyoyatenda katika madhambi.
Mafunzo
- Pupa ya Maswahaba katika kujua njia za kusalimika.
- Kumebainishwa sababu za kusalimika katika Dunia na Akhera.
- Himizo la mtu kushughulika na nafsi yake anaposhindwa kumnufaisha mtu mwingine, au akahofia madhara juu ya dini yake na nafsi yake endapo atachanganyikana na watu.
- Hapa kuna ishara ya kuipa kipaumbele nyumba, na hasa hasa wakati wa fitina, kwani ni katika nyenzo za kuihifadhi dini.
Ufafanuzi: العربية
سَأَلَ عُقبةُ بن عامر رضي الله عنه النبيَّ صلى الله عليه وسلم عن أسباب نَجاة المؤمن في الدنيا والآخرة؟ فقال صلى الله عليه وسلم: عليك بثلاثة أمور: الأول: احفظ لسانَك عمّا لا خير فيه، وعن قول كل شر، ولا تنطق إلا بخير. الثاني: الزم بيتَك لِتَعبد الله في الخلوات، واشتغل بطاعة الله عز وجل، واعتزل في بيتك عن الفتن. الثالث: ابْكِ واندَمْ وتُبْ ممّا ارتكبتَ مِن ذنوب.
- حرص الصحابة رضي الله عنهم على معرفة سُبُل النَّجَاة.
- بيان أسباب النجاة في الدنيا والآخرة.
- الحث على انشغال الإنسان بنفسه إذا عَجز عن نَفْع غيره، أو خاف الضرر على دِينه ونفسه إذا خالط الناس.
- الإشارة إلى الاهتمام بالبيت وخصوصًا عند الفتن، فهو من الوسائل لحفظ الدين.