Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
SahihiImepokelewa Imamu Muslim
Matini ya Kiarabu
عَنِ شُرَيْحٍ بنِ هانِئٍ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ، قُلْتُ: بِأَيِّ شَيْءٍ كَانَ يَبْدَأُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا دَخَلَ بَيْتَهُ؟ قَالَتْ: بِالسِّوَاكِ.
Tafsiri
Kutoka kwa Shuraihi bin Hanii amesema: Nilimuuliza Aisha, nikasema: Ni kwa jambo gani alikuwa akianza nalo Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia nyumbani kwake? Akasema: Kwa mswaki.
Ufafanuzi
Ilikuwa katika muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuanza na mswaki anapoingia nyumbani kwake wakati wowote, usiku au mchana.
Mafunzo
- Sheria ya kupiga mswaki ni ya ujumla kwa nyakati zote, na inatiwa mkazo: katika nyakati ambazo sheria imehimiza, miongoni mwake ni: Wakati wa kuingia nyumbani, na wakati wa swala, na wakati wa udhu, na baada ya kuamka kutoka usingizini, na wakati wa kubadilika kwa harufu ya kinywa.
- Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba ya kuuliza kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na sunna zake; ili wamuige.
- Kuchukua elimu kutoka kwa wenye elimu na kwa wale wenye kujua zaidi, kiasi ambacho aliulizwa Aisha kuhusu hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakati wa kuingia kwake nyumbani.
- Uzuri wa maisha ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake na familia yake, kiasi kwamba alikuwa akisafisha kinywa chake wakati wa kuingia.
Ufafanuzi: العربية
كَانَ مِن هَدِيِ النبيِّ صلى الله عليه وسلم أَنْ يَبدأ بالسواك إذا دَخل بيتَه في أيِّ وقتٍ ليلًا أو نهارًا.
- مشروعية السواك عامة في جميع الأوقات، ويتأكّد ذلك: في الأوقات التي نَدَبَ الشارع إليها، ومنها: عند دخول البيت، وعند الصلاة، وعند الوضوء، وبعد الاستيقاظ من النوم، وعند تَغَيُّر رائحة الفم.
- بيان حرص التابعين على السؤال عن أحوال النبيِّ صلى الله عليه وسلم وسُنَنِهِ؛ ليقتدوا به.
- أخْذ العلم من أهله وممن هو أَعْرف به، حيث سُئلت عائشة رضي الله عنها عن حال النبي صلى الله عليه وسلم عند دخول البيت.
- حسن معاشرة النبي صلى الله عليه وسلم لأهله، حيث كان يُطَهِّر فَمَه عند الدخول.