Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَسْتُرُ عَبْدٌ عَبْدًا فِي الدُّنْيَا إِلَّا سَتَرَهُ اللهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hatomsitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa Mwenyezi Mungu atamsitiri siku ya kiyama"
Ufafanuzi
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu hatomsitiri ndugu yake katika jambo miongoni mwa mambo, isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamsitiri siku ya Kiyama; kwani malipo huendana na matendo, na stara ya Mwenyezi Mungu kwake inakuwa kwa kuzisitiri aibu zake na maasi yake kwa kutoyatangaza mbele ya umati wa siku ya Kiyama, na huenda inawezakuwa kwa kutoyahesabu na kutomkumbusha.
Mafunzo
- Sheria ya kumsitiri muislamu anapofanya maasi, pamoja na kumkemea, na kumnasihi, na kumhofisha kwa Mwenyezi Mungu, ama akiwa ni katika watu wa shari na uovu wenye kutangaza wazi maasi na uovu, hawa haitakiwi kusitiriwa; kwa sababu kuwasitiri kunawapa ujasiri wa kufanya maasi, bali wanatakiwa kushitakiwa katika mamlaka husika, hata kama watatajwa kwa majina; kwa sababu mtu anakuwa katangaza wazi yeye mwenyewe maovu yake na maasi yake.
- Himizo la kusitiri aibu za watu wengine.
- Miongoni mwa faida za kusitiri: Ni kumpa fursa mkosefu ya kuirejea nafsi yake na atubie kwa Mwenyezi Mungu; kwa sababu kutangaza aibu na fedhehe ni katika kueneza maovu, na kunaharibu hali ya hewa ya jamii, na kunawahadaa watu kuendelea kuyatenda.
Ufafanuzi: العربية
يُبَيِّنُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنه لا يَستر مسلمٌ أخاه المسلم في أمر من الأمور، إلا سَتره الله عز وجل يوم القيامة؛ فالجزاء من جنس العمل، ويكون سِتْرُ اللهِ له بستر عيوبه ومعاصيه عن إذاعتها على أهل المحشر، وقد يكون بترك محاسبته عليها وذكرها له.
- مشروعية السِّتْر على المسلم إذا فَعَلَ معصية، مع الإنكار عليه، والنصيحة له، وتخويفه بالله، أما إذا كان من أهل الشر والفساد المجاهرين بالمعاصي والفسق، فإنه لا ينبغي الستر عليهم؛ لأن الستر عليهم يُجَرِّئُهم على المعاصي، وإنما يُرْفَع أمرُه إلى ولاة الأمور، ولو كان في هذا ذكر له؛ لأنه مُعْلِن بفسقه ومعصيته.
- الترغيب في ستر أخطاء الآخرين.
- من فوائد الستر: إتاحة الفرصة للمذنب أن يراجِعَ نفسه ويتوب إلى الله؛ لأن إعلان العيوب والعورات من إشاعة الفاحشة، ويُفسِد الجَوَّ الاجتماعي، ويُغْرِي الناس بارتكابها.