Hadithi

Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يَبْسُطُ يَدَهُ بِاللَّيْلِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ النَّهَارِ، وَيَبْسُطُ يَدَهُ بِالنَّهَارِ لِيَتُوبَ مُسِيءُ اللَّيْلِ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ مِنْ مَغْرِبِهَا».

Tafsiri

Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: "Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake wakati wa usiku ili amsamehe mkosefu wa mchana, na ananyoosha mkono wake wakati wa mchana ili amsamehe mkosaji wa usiku, mpaka jua litakapochomoza kutoka magharibi yake."

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anakubali toba kutoka kwa waja wake, mja akitenda dhambi wakati wa mchana na akatubia usiku Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, na akitenda dhambi usiku na akatubia mchana basi Mwenyezi Mungu hukubali toba yake, Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ananyoosha mkono wake kwa kuifurahia toba, na kuikubali, na mlango wa toba unabaki wazi mpaka jua lichomoze kutoka magharibi, likiashiria mwisho wa dunia, basi likichomoza mlango wa toba utafungwa.

Mafunzo

  • Kukubaliwa toba kunaendelea maadamu mlango wake uko wazi, na mlango wake utafungwa wakati jua linapochomoza kutoka magharibi, na kwamba mtu atubu kabla ya msukosuko wa kifo, ambao ni roho kufika kooni.
  • Kutokata tamaa kwa sababu ya dhambi, kwani msamaha na rehema za Mwenyezi Mungu ni mpana, na mlango wa toba uko wazi.
  • Masharti ya kutubia: La kwanza: kuacha dhambi, la pili: kujuta kwa kuitenda, na la tatu: kuazimia kutorejea tena, ikiwa ni katika haki za Mwenyezi Mungu, na ikiwa inahusiana na haki za waja, basi kwa ajili ya kupokelewa toba inatakiwa kuwa haki hiyo apewe mmiliki wake au mwenye haki amsamehe.
Ufafanuzi: العربية

يُخبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم: أنَّ الله تعالى يقبل التوبة من عباده، فإن أذنب العبد ذنبًا بالنهار وتاب بالليل قَبِلَ الله توبته، وإن أذنب ذنبًا بالليل وتاب بالنهار قَبل الله توبته، ويبسط يده سبحانه للتوبة فرحًا بها، وقبولًا لها، ولا يزال باب التوبة مفتوحًا حتى تطلع الشمس من مغربها إيذانًا بانتهاء الدنيا، فإذا طلعت فإن باب التوبة يُغلق.

  • قبول التوبة مستمر ما دام بابها مفتوحًا، ويغلق بابها بمطلع الشمس من مغربها، وأن يتوب الإنسان قبل غرغرة الموت، وهي وصول الروح إلى الحلقوم.
  • عدم اليأس والقنوط بسبب الذنب، فإن عفو الله سبحانه ورحمته واسعة، وباب التوبة مفتوح.
  • شروط التوبة: الأول: الإقلاع عن المعصية، والثاني: الندم على فعلها، والثالث: العزم على ألّا يعود إليها أبدًا، هذا إن كانت في حقوق الله تعالى، وإن كانت متعلِّقة بحق من حقوق العباد، فيشترط لصحة التوبة أن يؤدي ذلك الحق إلى صاحبه، أو يعفو عنه صاحب الحق.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi