Hadithi

Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad

Matini ya Kiarabu

عَنْ زِرِّ بْنِ حُبَيْشٍ قَالَ: أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ المُرَادِيَّ، أَسْأَلُهُ عَنِ المَسْحِ عَلَى الخُفَّيْنِ، فَقَالَ: مَا جَاءَ بِكَ يَا زِرُّ؟ فَقُلْتُ: ابْتِغَاءَ العِلْمِ، فَقَالَ: إِنَّ المَلاَئِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ العِلْمِ؛ رِضًا بِمَا يَطْلُبُ، فَقُلْتُ: إِنَّهُ حَكَّ فِي صَدْرِي المَسْحُ عَلَى الخُفَّيْنِ بَعْدَ الغَائِطِ وَالبَوْلِ، وَكُنْتَ امْرَأً مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَجِئْتُ أَسْأَلُكَ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي ذَلِكَ شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كَانَ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا سَفْرًا أَوْ مُسَافِرِينَ أَلَّا نَنْزِعَ خِفَافَنَا ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيهِنَّ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ، لَكِنْ مِنْ غَائِطٍ وَبَوْلٍ وَنَوْمٍ، فَقُلْتُ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي الهَوَى شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ فَبَيْنَا نَحْنُ عِنْدَهُ إِذْ نَادَاهُ أَعْرَابِيٌّ بِصَوْتٍ لَهُ جَهْوَرِيٍّ: يَا مُحَمَّدُ، فَأَجَابَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى نَحْوٍ مِنْ صَوْتِهِ: «هَاؤُمُ» وَقُلْنَا لَهُ: وَيْحَكَ اغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ، فَإِنَّكَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَدْ نُهِيتَ عَنْ هَذَا، فَقَالَ: وَاللَّهِ لاَ أَغْضُضُ، قَالَ الأَعْرَابِيُّ: المَرْءُ يُحِبُّ القَوْمَ وَلَمَّا يَلْحَقْ بِهِمْ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ يَوْمَ القِيَامَةِ»، فَمَا زَالَ يُحَدِّثُنَا حَتَّى ذَكَرَ بَابًا مِنْ قِبَلِ المَغْرِبِ مَسِيرَةُ عَرْضِهِ، أَوْ يَسِيرُ الرَّاكِبُ فِي عَرْضِهِ أَرْبَعِينَ أَوْ سَبْعِينَ عَامًا.

Tafsiri

Kutoka kwa Zirri bin Hubaishi amesema: Nilikwenda kwa Swafwan bin Assali Al-Muraadi, ili nimuulize kuhusu kufuta juu ya khofu mbili, akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Nikasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kile anachokitafuta, basi nikasema: Hakika mimi nimepata uzito ndani ya kifua changu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya kukidhi haja ndogo na kubwa, na wewe ulikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hivyo nimekuja kukuuliza: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu hilo? Akasema: Ndiyo, Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu matamanio? Akasema: Ndiyo, tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiendelea kuwa naye ghafla, Bedui mmoja alimuita kwa sauti kubwa na ya juu. Ewe Muhammadi!!!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa mfano wa sauti yake: "Ehee, niambie!" Tukasema kumwambia koma!, punguza sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kufanya hivi, akasema: Wallahi siwezi kupunguza, kisha Bedui akasema: Utakuta mtu anawapenda watu fulani lakini hajawahi kukutana nao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda siku ya Kiyama" Basi akaendelea kutusimulia mpaka akautaja mlango ulioko Magharibi mwendo wa upana wake, au anaweza kutembea aliyepanda kwenye upana wake kwa miaka arobaini au sabini.

Ufafanuzi

Alikuja Zirri bin Hubaishi kwa Swafwan bin Assali radhi za Allah ziwe juu yake, ili amuulize kuhusu khofu mbili, Swafwan akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Akasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kutukuza kile anachokifanya mwenye kutafuta elimu, Zirii akasema: Hakika nimepata shaka ndani ya nafsi yangu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya haja kubwa na ndogo, na wewe ni katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nimekuja hapa kukuuliza, je, uliwahi kumsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitaja chochote kuhusu hili?. Akasema Swafwan: Ndiyo, alikuwa akituamrisha tunapokuwa wasafiri tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) kwa sababu ya hadathi (uchafu) mdogo, kama haja kubwa na ndogo na usingizi, isipokuwa janaba hapo basi ni wajibu kuvua, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu mapenzi? Akasema: Ndiyo: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiwa bado tuko pamoja naye mara ghafla Bedui mmoja aliita kwa sauti ya juu sana: Ewe Muhammadi!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa sauti ya juu karibu na sauti yake: Njoo, nasi tukasema kumwambia: Koma! Shusha sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kunyanyua sauti mbele yake. Akasema kwa sababu ya ukaidi wake: Wallahi siwezi kuishusha, Bedui akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, utakuta mtu anawapenda watu wema na hajafanya matendo mfano wa matendo yao? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtu atakuwa pamoja na anayempenda siku ya Kiyama, Anasema Zirri: Swafwan akaendelea kutuhadithia mpaka akataja mlango wa toba ulioko upande wa Sham aliuumba Mwenyezi Mungu siku aliyoumba Mbingu na Ardhi, anaweza kutembea aliyepanda juu ya kipando kwenye upana wake miaka arobaini au sabini, na wala haufungwi mpaka Jua lichomoze kutokea Magharibi yake.

Mafunzo

  • Ubora wa kutafuta elimu, na nafasi ya mwenye kutafuta elimu, na Malaika kumfunika.
  • Kumebainishwa pupa ya wanafunzi wa Maswahaba katika kutafuta elimu kutoka kwa Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao.
  • Kufaa kufuta juu ya khofu mbili, na muda wake: Kwa msafiri ni siku tatu (ikiwa ni pamoja na usiku wake), na kwa mkazi siku moja (masaa 24).
  • Kufuta khofu mbili kunakuwa katika hadathi ndogo pekee.
  • Inafaa kwa muulizaji kumuomba msomi ushahidi wa kile alichozungumza, je ni nukuu za maandiko au ni jitihada zake, na kwa msomi asijisikie vibaya kwa hilo.
  • Kuwa na adabu na wanachuoni na watu wema, na kushusha sauti katika vikao vya kielimu.
  • Kumfundisha asiyejua adabu nzuri na misingi ya tabia njema.
  • Himizo la kujifunza kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika upole wake, na tabia zake njema, na kuzungumza kwake na watu kulingana na uelewa wao na akili zao.
  • Amesema Mubaarakafuri: Hapa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alinyanyua sauti yake kama sehemu ya kumhurumia ili zisiporomoke amali zake kutokana na kauli yake Mtukufu: "Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii"; akampa udhuru kwa sababu ya ujinga wake, na alinyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake sauti yake mpaka ikawa mfano wa sauti yake au juu yake zaidi kwa sababu ya huruma yake iliyopita kiasi kwake.
  • Kuwa na pupa ya kukaa na watu wema na kuwa karibu nao na kuwapenda.
  • Amesema Nawawi: Na si lazima mtu kuwa nao mpaka daraja yake na malipo yake yawe mfano wao kwa namna zote.
  • Kufungua mlango wa matumaini na matarajio, na kutoa habari njema ya kusalimika, na kuwa mpole katika mawaidha.
  • Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na kufungua kwake mlango wa toba.
  • Himizo la kufanya haraka kuomba toba na kuihesabu nafsi na kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ufafanuzi: العربية

جاء زرّ بن حبيش إلى صفوان بن عَسّال رضي الله عنه، يسأله عن المسح على الخفين، فقال صفوان: ما جاء بك يا زر؟ فقال زر: ابتغاء العلم، فقال: إن الملائكة لتضع أجنحتها لطالب العلم؛ رضًا وتعظيمًا لما يفعل طالب العلم، فقال زر: إنه تردد في نفسي المسح على الخفين بعد الغائط والبول، وأنت من أصحاب النبي صلى الله عليه وسلم وجئت أسألك هل سمعت النبي يذكر في ذلك شيئًا؟ قال صفوان: نعم، كان يأمرنا إذا كنا مسافرين ألَّا ننزع خفافنا ثلاثة أيام بلياليهن من الحدث الأصغر كغائط وبول ونوم، إلا الجنابة فيجب النزع إذن، فقلت: هل سمعته يذكر في الحُب شيئًا؟ قال: نعم، كنا مع النبي صلى الله عليه وسلم في سفر فبينا نحن عنده إذ ناداه أعرابي بصوت عالٍ: يا محمد، فأجابه صلى الله عليه وسلم بصوت عالٍ قريبًا من صوته: تعال، وقلنا له: ويلك اخفض صوتك، فإنك عند النبي صلى الله عليه وسلم، وقد نهيت عن رفع الصوت عنده. فقال لغلظته: والله لا أخفضه، قال الأعرابي: يا رسول الله المرء يحب القوم الصالحين ولم يعمل بمثل عملهم؟ قال النبي صلى الله عليه وسلم: المرء مع من أحب يوم القيامة، قال زر: فما زال صفوان يحدثنا حتى ذكر بابًا للتوبة من جهة الشام خلقه الله يوم خلق السماوات والأرض يسير الراكب في عرضه أربعين أو سبعين عامًا، ولا يغلق حتى تطلع الشمس من مغربها.

  • فضل طلب العلم، وعظم منزلة طالب العلم، واحتفاء الملائكة به.
  • بيان حرص التابعين على طلب العلم من الصحابة رضي الله عنهم.
  • جواز المسح على الخفين، ومدته: للمسافر ثلاثة أيام بلياليها، وللمقيم يوم وليلة.
  • مسح الخفين يكون في الحدث الأصغر فقط.
  • جواز مطالبة السائل للعالم عن دليله أهو نص أم استدلال واجتهاده، وعلى العالم ألَّا يتحرج من ذلك.
  • التأدب مع العلماء والصالحين، وخفض الصوت في مجالس العلم.
  • تعليم الجاهل حسن الأدب وقواعد السلوك.
  • الحث على الاقتداء بالنبي صلى الله عليه وسلم في حِلْمه، وحسن خلقه، ومخاطبته الناس على قدر علمهم وعقولهم.
  • قال المباركفوري: وإنما رفع صوته عليه الصلاة والسلام من طريق الشفقة عليه لئلا يحبط عمله من قوله تعالى: {لَا ‌تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ}؛ فعذره لجهله، ورفع النبي صلى الله عليه وسلم صوته حتى كان مثل صوته أو فوقه لفرط رأفته به.
  • الحرص على مجالسة الصالحين والقرب منهم وحبهم.
  • قال النووي: ولا يلزم من كونه معهم أن تكون منزلته وجزاؤه مثلهم من كل وجه.
  • فتح باب الأمل والرجاء، والتبشير بالنجاة، واللطف في الموعظة.
  • سعة رحمة الله عز وجل، وفتحه باب التوبة.
  • الحث على الإسراع في التوبة ومحاسبة النفس والرجوع إلى الله تعالى.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi