Hadithi

Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Imamu Ahmad, Tirmidhiy, Nasai na Ibn Majah

Matini ya Kiarabu

عَنْ المِقْدَامِ بْنِ مَعْدِي كَرِبَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَا مَلأَ آدَمِيٌّ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنٍ، بِحَسْبِ ابْنِ آدَمَ أَكَلاَتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ، فَإِنْ كَانَ لَا مَحَالَةَ، فَثُلُثٌ لِطَعَامِهِ، وَثُلُثٌ لِشَرَابِهِ، وَثُلُثٌ لِنَفَسِهِ».

Tafsiri

Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Karibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake".

Ufafanuzi

Anatuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika msingi miongoni mwa misingi ya tiba, nayo ni kinga ambayo mtu analinda kwayo afya yake, ambayo ni kupunguza kula, bali ale kwa kiasi cha kuziba tumbo lake na kupata nguvu ya kufanya kazi zake za lazima, na hakika chombo cha shari zaidi kilichowahi kujazwa ni tumbo, na hii ni kwa sababu ya matokeo ya shibe, kama maradhi mabaya yasiyohesabika yanayokuja haraka au kwa baadaye, ya siri au ya wazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ikiwa mtu hana namna zaidi ya kushiba, basi afanye kula kuwe kwa kiasi cha theluthi, na theluthi nyingine ya kinywaji, na theluthi nyingine ya pumzi ili asipate dhiki na madhara, na uvivu wa kutekeleza aliyomuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yake katika swala la dini yake au dunia yake.

Mafunzo

  • Kutozidisha katika kula na kunywa, na huu ni msingi unaokusanya misingi yote ya tiba, kwa kuwa katika kuzidisha kula kuna maradhi na magonjwa.
  • Lengo la kula, ni kuhifadhi afya na nguvu ambayo ndio usalama wa maisha.
  • Kujaza tumbo kwa chakula kuna madhara ya mwili na ya dini, amesema Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tahadharini na kuvimbewa, kwani ni madhara kwa mwili na hutia uvivu wa kuswali".
  • Kula kwa mujibu wa hukumu kuna gawanyika: 1- Wajibu: Nako ni kule kunakohifadhi uhai na kuacha kwake kunaweza kupelekea madhara. 2- Inafaa: Nako ni kule kunakozidi katika kiwango cha wajibu na wala hakuna madhara kama ataacha. 3- Inachukiza: Nako ni kule kunakohofiwa madhara. 4- Haramu: Nako ni kule kunakojulikana kuwa kuna madhara. 5- Inapendeza: Nako ni kule kunakoweza kuwa msaada wa kufanya ibada na kumtii Mwenyezi Mungu, na imekusanywa vizuri katika hadithi katika daraja tatu: Ya kwanza: Kujaza tumbo. Ya pili: Matonge kadhaa yanayoweza kumpa nguvu ya kusimama. Ya tatu: Kauli yake: "Theluthi moja iwe kwa ajili ya chakula chake na theluthi nyingine kwa ajili ya kinywaji chake na theluthi nyingine kwa ajili ya pumzi yake" Na hii yote ikiwa kama aina ya chakula ni cha halali.
  • Hadithi hii ni kanuni miongoni mwa kanuni za tiba, kiasi ambacho hata elimu ya udaktari inazunguka katika misingi mitatu: Kuhifadhi nguvu, na kuilinda, na kuacha nafasi ya kupumua, hadithi imekusanya mambo mawili ya mwanzo katika hayo, kama ilivyokuja katika kauli yake Mtukufu: "Na kuleni na mnywe wala msifanye fujo kwani hakika Yeye hawapendi wafanyao fujo" [Al-Araf: 31].
  • Ukamilifu wa sheria hii, kiasi ambacho imekusanya masilahi yote ya mwanadamu katika dini yake na dunia yake.
  • Miongoni mwa elimu za sheria ni misingi ya udaktari na aina zake, kama ilivyokuja katika Asali na Habbati Saudaa.
  • Hukumu za sheria kujawa na hekima, na kwamba zimejengeka katika kuzuia madhara na kuleta manufaa.
Ufafanuzi: العربية

يرشدنا النبي الكريم صلى الله عليه وسلم إلى أصل من أصول الطب، وهي الوقاية التي يقي بها الإنسان صحته، وهي التقليل من الأكل، بل يأكل بقدر ما يسد رمقه ويقويه على أعماله اللازمة، وإن شر وعاء مُلئ هو البطن لما ينتج عن الشبع من الأمراض الفتاكة التي لا تحصى عاجلًا أو آجلًا باطنًا أو ظاهرًا. ثم إن الرسول صلى الله عليه وسلم قال: إذا كان الإنسان لابد له من الشبع، فليجعل الأكل بمقدار الثلث، والثلث الآخر للشرب، والثلث للنفس حتى لا يحصل عليه ضيق وضرر، وكسل عن تأدية ما أوجب الله عليه في أمر دينه أو دنياه.

  • عدم التوسع في الأكل والشرب، وهذا أصل جامع لأصول الطب كلها، لما في كثرة الشبع من الأمراض والأسقام.
  • الغاية من الأكل، هي حفظ الصحة والقوة وبهما سلامة الحياة.
  • لملء البطن من الطعام أضرار بدنية ودينية، قال عمر رضي الله عنه: «إياكم والبطنة، فإنها مفسدة للجسم ومكسلة عن الصلاة».
  • الأكل من حيث الحكم على أقسام: واجب، وهو ما به تُحفظ الحياة ويؤدي تركه إلى ضرر. جائز، وهو ما زاد على القدر الواجب ولا يُخشى ضرره. مكروه، وهو ما يُخشى ضرره. محرم، وهو ما يُعلم ضرره. ومستحب، وهو ما يُستعان به على عبادة الله وطاعته، وقد أجمل ذلك في الحديث في ثلاث مراتب: أولها: ملء البطن. ثانيها: أكلات أو لقيمات يقمن صلبه. ثالثها: قوله: «ثلث لطعامه وثلث لشرابه وثلث لنفسه» وهذا كله إذا كان جنس المأكول حلالًا.
  • الحديث قاعدة من قواعد الطب، وحيث إن علم الطب مداره على ثلاثة أصول: حفظ القوة والحمية والاستفراغ، فقد اشتمل الحديث على الأولين منها، كما في قوله تعالى : (وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ) [الأعراف: 31].
  • كمال هذه الشريعة حيث اشتملت على مصالح الإنسان في دينه ودنياه.
  • من علوم الشريعة أصولُ الطب وأنواع منه، كما جاء في العسل والحبة السوداء.
  • اشتمال أحكام الشريعة على الحكمة، وأنها مبنية على درء المفاسد وجلب المصالح.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi