Hadithi

hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَن أَبِي بُرْدَةَ بْنِ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: وَجِعَ أَبُو مُوسَى وَجَعًا شَدِيدًا، فَغُشِيَ عَلَيْهِ وَرَأْسُهُ فِي حَجْرِ امْرَأَةٍ مِنْ أَهْلِهِ، فَلَمْ يَسْتَطِعْ أَنْ يَرُدَّ عَلَيْهَا شَيْئًا، فَلَمَّا أَفَاقَ، قَالَ: أَنَا بَرِيءٌ مِمَّنْ بَرِئَ مِنْهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَرِئَ مِنَ الصَّالِقَةِ وَالحَالِقَةِ وَالشَّاقَّةِ.

Tafsiri

Kutoka kwa Abuu Burda bin Abii Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Aliumia Abuu Mussa maumivu makali, akazimia na kichwa chake kikiwa katika paja la mwanamke katika wake zake, akawa hakuweza kumjibu chochote, alipozinduka, akasema: Mimi najitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hakika Mtume rehema na amani ziwe juu yake alijitenga mbali na mpiga mayowe, na mnyoa nywele, na mchana nguo.

Ufafanuzi

Amesimulia Abuu Burda radhi za Allah ziwe juu yake kuwa baba yake Abuu Mussa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake aliugua maradhi makali, akazimia, na kichwa chake kilikuwa katika paja la mwanamke mmoja katika wake zake, akapiga mayowe yule mwanamke kwa kumuita, akawa hakuweza kumjibu chochote kwa sababu ya kuzimia kwake. Alipozinduka akasema kuwa: Hakika yeye anajitenga mbali na yule aliyejitenga mbali naye Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na hakika yeye rehema na amani ziwe juu yake alijitenga naye. Mpiga mayowe: Naye ni mwanamke anayenyanyua sauti yake wakati wa msiba. Na mnyoaji: Ni mwanamke anayenyoa nywele zake wakati wa msiba. Na mchana nguo: Ni mwanamke anayechana nguo zake wakati wa msiba. Kwa sababu haya ni katika mambo ya zama za ujinga, bali aliamrisha kuwa na subira wakati wa msiba, na kutaraji malipo yake kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo

  • Katazo la kuchana nguo, na kunyoa nywele, na kunyanyua sauti wakati wa kutokea misiba, nakuwa hilo ni katika madhambi makubwa.
  • Huzuni na kulia pasina maombolezo na kunyanyua sauti si haramu, hili halipingani na subira juu ya maamuzi ya Mwenyezi Mungu, bali ni rehema.
  • Uharamu wa kulalamika katika makadirio ya Mwenyezi Mungu yenye kuumiza kwa kauli au vitendo.
  • Uwajibu wa kuwa na subira wakati wa misiba.
Ufafanuzi: العربية

حَكَى أبو بردة رضي الله عنه أنّ أباه أبا موسى الأشعري رضي الله عنه مَرض مرضًا شديدًا فأغمي عليه، وكانت رأسه في حِجْر امرأةٍ من أهله، فصاحت ونَدَبَتْه، فلم يستطع أن يَرُدَّ عليها شيئًا بسبب إغمائه. فلما أفاق قال: إنه بريءٌ ممن بَرِئَ منه رسول الله صلى الله عليه وسلم، وإنه صلى الله عليه وسلم قد بَرِئَ من: الصالقة: وهي الرافعة صوتها عند المصيبة. والحالقة: وهي التي تَحلق شعرها عند المصيبة. والشاقة: وهي التي تَشقُّ ثوبها عند المصيبة. لأنها من أمور الجاهلية، بل أمر بالصبر عند المصائب، واحتساب أجرها على الله.

  • النهي عن شَقِّ الثوب، وحَلْق الشعر، ورفع الصوت عند وقوع المصائب، وأن ذلك من كبائر الذنوب.
  • الحزن والبكاء دون نياحةٍ ورَفْعِ صوتٍ ليس محرّمًا، فهو لا ينافي الصبر على قضاء الله، وإنما هو رحمة.
  • تحريم التسخُّط من أقدار الله المؤلمة بالقول أو الفعل.
  • وجوب الصبر عند وقوع المصائب.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi