Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «كلُّ بني آدم خَطَّاءٌ، وخيرُ الخَطَّائِينَ التوابون».
Tafsiri
Kutoka kwa Anas bin Malik- Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Allah- Rehma na amani ziwe juu yake- "Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia".
Ufafanuzi
Haepukani mwanadamu na kukosea, kwa jinsi alivyoumbwa kutokana na udhaifu, na kutokumtii msimamizi wake katika kutekeleza yale aliyomtaka ayafanye, na kuacha yale aliyomkataza, lakini yeye Mtukufu amefungua mlango wa toba kwa waja wake, na akaeleza kuwa mbora wa wakosefu ni wale wenye kukithirisha toba.
Mafunzo
- Katika mambo ya mwanadamu ni kukosea na kuingia katika dhambi. La msingi kwa muumini atakapojiiingiza katika maasi afanye haraka kuleta toba.
Ufafanuzi: العربية
لا يخلو الإنسان من الخطيئة، لما فُطر عليه من الضعف، وعدم الانقياد لمولاه في فعل ما دعاه إليه، وترك ما نهاه عنه، لكنه تعالى فتح باب التوبة لعباده، وأخبر أن خير الخطائين هم المكثرون من التوبة.
- من شأن ابن آدم الخطأ والوقوع في الذنب.
- الواجب على المؤمن إذا تلبس بمعصية أن يبادر بالتوبة.