Hadithi

Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عن عائشة رضي الله عنها قالت: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «لَا تَسُبُّوا الْأَمْوَاتَ، فَإِنَّهُمْ قَدْ أَفْضَوْا إِلَى مَا قَدَّمُوا».

Tafsiri

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo mazuri au mabaya, kama ambavyo matusi haya hayawafikii basi hakuna lolote zaidi ya kuwaudhi waliohai.

Mafunzo

  • Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.
  • Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.
  • Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.
  • Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.
Ufafanuzi: العربية

يُبَيِّنُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم حُرْمةَ سبِّ الأموات والوقوع في أعراضهم، وأنَّ هذا من مَسَاوِئ الأخلاق، فإنهم وَصَلُوا إلى ما قدَّموه من أعمال صالحة أو طالحة، وكما أنّ هذا السبَّ لا يبلغهم فإنّه إنما يؤذي الأحياء.

  • الحديث دليل على تحريم سب الأموات.
  • ترك سب الأموات فيه مراعاة لمصلحة الأحياء، والحفاظ على سلامة المجتمع من التشاحن والتباغض.
  • الحكمة من النهي عن سبهم أنهم وصلوا إلى ما قدموا فلا ينفع سبهم، وفيه إيذاء لأقاربه الأحياء.
  • أنه لا ينبغي للإنسان أن يقول ما لا مصلحة فيه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi