Hadithi

Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ غَدَا إِلَى الْمَسْجِدِ أَوْ رَاحَ أَعَدَّ اللهُ لَهُ فِي الْجَنَّةِ نُزُلًا، كُلَّمَا غَدَا أَوْ رَاحَ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayekwenda asubuhi msikitini au mchana, Mwenyezi Mungu humuandalia nyumba peponi kila anapotoka asubuhi au jioni"

Ufafanuzi

Amempa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kwenda msikitini kwa ajili ya ibada au elimu kwa lengo jingine katika mambo ya kheri katika wakati wowote; mwanzo wa mchana au mwisho wake kuwa Mwenyezi Mungu amemuandalia mahali na takrima ya ugeni peponi, kila anapokuja msikitini usiku au mchana.

Mafunzo

  • Fadhila za kwenda msikitini, na himizo la kuhifadhi swala ya jamaa ndani ya msikiti, kwani anapitwa na daraja ngapi mwenye kukwepa kwenda msikitini na kheri na fadhila na malipo na ugeni aliouandaa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye kwenda katika nyumba yake.
  • Ikiwa watu humkirimu anayewajia katika majumba yao, na kumletea chakula, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu ni mkarimu zaidi kuliko viumbe wake! Yeyote atakayekwenda katika nyumba yake basi atamkirimu, na Mwenyezi Mungu atamuandalia mafikio ya thamani na yenye nafasi kubwa.
  • Furaha na moyo mkunjufu wakati wa kwenda msikitini; kwa sababu anaandaliwa makazi kila anapokwenda asubuhi au mchana kwa idadi ya kwenda kwake.
Ufafanuzi: العربية

بَشَّرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم مَن أتى المَسجدَ للعبادة أو العلم أو لغير ذلك مِن مقاصد الخير في أيِّ وقت؛ أولَ النهار أو آخرَه بأنَّ الله قد هَيَّأَ له مَكانًا وضِيافة في الجنة، كلّما جاء المسجد في ليل أو نهار.

  • فَضْل الذهاب إلى المسجد، والحَثُّ على المحافظة على صلاة الجماعة فيه، فَكَم يَفُوْتُ المُتَخَلِّف عن المساجد من الخير والفضل والأجر والضيافة التي يعدُّها الله تبارك وتعالى لقاصِدِيْ بيته.
  • إذا كان الناس يُكرِمُون من جاء بيوتَهم، ويُقَدِّمون له الطعام، فالله تبارك وتعالى أَكْرَمُ مِن خَلْقِه! فمَن قَصَدَ بيتَه أَكرمَه، وأَعَدّ الله له نزلًا عظيمًا وكبيرًا.
  • الفرح والغِبْطَة بالذهاب للمساجد؛ لأنه يُعَدّ له نُزُلٌ كلّما غَدَا أو رَاح بِعَدَد ذهابِه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi