Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن علي رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «رُفِعَ الْقَلَمُ عن ثلاثة: عن النائم حتى يَسْتَيْقِظَ، وعن الصبي حتى يَحْتَلِمَ، وعن المجنون حتى يَعْقِلَ».
Tafsiri
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Ufafanuzi
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kubeba wajibu ni lazima kwa mwanadam isipokuwa hawa watatu: Mtoto mdogo mpaka akue na abalehe. Na kwa mwendawazimu aliyepoteza akili mpaka akili irudi. Na kwa aliyelala mpaka aamke. Kubeba wajibu kumeondolewa kwao, na kutenda kwao madhambi hakuandikwi, lakini mtoto huandikiwa kheri anapofanya, isipokuwa mwendawazimu na aliyelala; kwa sababu wote hawa wako katika kundi la mtu asiyekubalika ibada yake kwa kupoteza hisia.
Mafunzo
- Kupoteza uwezo wa mtu hutokea ima kwa sababu ya usingizi, ambao unamzuia kuwa na uwezo wa kuwa macho ili kutekeleza wajibu wake, au kwa sababu ya umri wake mdogo na utoto, ambao unamfanya kupoteza uwezo, au kwa sababu ya wendawazimu ambao huvuruga kazi za akili yake, au kinachofananishwa na hayo kama vile ulevi, atakayepoteza uwezo sahihi wa kupambanua na kufikiri, akakosa sifa kwa sababu ya sababu hizi tatu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uadilifu Wake na upole wake na ukarimu Wake amemuondolea dhambi kwa yale yanayotokea kwa makusudi au uzembe katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Kutoandika dhambi zao hakufuti baadhi ya hukumu za kidunia dhidi yao; kama mwendawazimu akiua, hakuna kisasi wala kafara kwake, na mtu wake mwenye akili timamu lazima alipe fidia.
- Kubalehe kuna dalili tatu: Kutokwa na manii, kwa kujiotea au kwa kinginecho, au kuota nywele sehemu za siri, au kutimiza miaka kumi na tano, na linaongezeka jambo la nne kwa mwanamke: nalo ni hedhi.
- Amesema Al-Subki: Mtoto kijana, na wengine wakasema: Mtoto aliye tumboni mwa mama yake anaitwa kijusi, akizaliwa anaitwa mvulana, na akiachishwa kunyonya, basi ni mvulana mpaka saba, basi anakuwa kijana mpaka kumi, kisha mdogo hadi kumi na tano, na kilicho yakini ni kwamba anaitwa mvulana katika matukio yote haya, alisema Al-Suyuti.
Ufafanuzi: العربية
أَخْبَرَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بأنَّ التكليفَ لازِمٌ لبني آدم إلا هؤلاء الثلاثة: الطفل الصغير حتى يَكْبُرَ ويَبْلُغ. وعن المجنون فاقِدِ العقل حتى يَرجِعَ إليه عقلُه. وعن النائم حتى يَستيقظَ. فالتكليف قد رُفِع عنهم، وفِعْلُهم الإثمَ لا يُكتبُ عليهم، لكن يُكتب الخيرُ للصبي الصغير دون المجنون والنائم؛ لأنهما في حَيِّزِ مَن ليس قابلًا لصحة العبادة منه لزوال الشعور.
- فَقْدُ الإنسانِ الأهليةَ يكون إما بسبب النوم الذي أفقده الاستيقاظَ لأداءِ واجباته، أو بسبب حَدَاثَةِ السِّنِّ والصِّغَرِ الذي هو معها فاقد للأهلية، أو بسبب الجنون الذي اضطربت معه وظائفه العقلية، أو ما يَلْحَق به كالسُّكْر، فمن فقد التمييز والتصوُّر الصحيحين، فانتفت عنه الأهلية بسببٍ من هذه الأسباب الثلاثة؛ فإن الله تبارك وتعالى بعدله، وحلمه، وكرمه، قد رَفَعَ عنه المؤاخذةَ بما يَصْدُرُ عنه من تعدٍّ أو تقصير في حق الله تعالى.
- عدم كتابة الآثام عليهم، لا ينافي ثبوت بعض الأحكام الدنيوية عليهم؛ كالمجنون لو قَتَل، فلا قود عليه ولا كفارة، وعلى عاقلته الدية.
- للبلوغ ثلاث علامات: نزولُ المنيِّ، باحتلام وغيره، أو نَباتُ شَعَر العَانة، أو بإتمام خمسة عشر عامًا، وتزيد المرأة أمرًا رابعًا: وهو الحيضُ.
- قال السبكي: الصبي الغلام، وقال غيره: الولد في بطن أمه يسمى جَنينًا فإذا وُلِد فصبيٌّ فإذا فُطِمَ فغلامٌ إلى سَبْعٍ ثم يَصيْرُ يافِعًا إلى عَشْر ثم حزورًا إلى خمس عشرة، والذي يُقطع به أنه يُسمّى صبيًّا في هذه الأحوال كلها، قاله السيوطي.