Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ يَزِيدَ الخَطْمِيِّ قَالَ: حَدَّثَنِي البَرَاءُ وَهُوَ غَيْرُ كَذُوبٍ، قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَالَ: سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ، لَمْ يَحْنِ أَحَدٌ مِنَّا ظَهْرَهُ حَتَّى يَقَعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ سَاجِدًا، ثُمَّ نَقَعُ سُجُودًا بَعْدَهُ.
Tafsiri
Kutoka kwa Abdallah bin Yazidi Al-Khatmiy amesema: Alinisimulia Al-Baraa naye si mtu wa kukadhibishwa, akasema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaposema: Sami'allaahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi) alikuwa hanyanyui yeyote miongoni mwetu mgongo wake mpaka aporomoke Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusujudu, kisha nasi tunaporomoka baada yake.
Ufafanuzi
Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Allah ziwe juu yake naye ni mkweli, ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaponyanyua kichwa chake kutoka katika rukuu anasema: Sami'allahu liman hamidah: (Amemsikia Mwenyezi Mungu mwenye kumhimidi), walikuwa wakiendelea kusimama walioko nyuma yake, na hainamishi yeyote miongoni mwao mgongo wake kwa ajili ya kusujudu mpaka aweke rehema na amani ziwe juu yake paji lake la uso katika Ardhi, kisha wanaporomoka wote kwa kusujudu baada yake.
Mafunzo
- Namna Maswahaba walivyomfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala, nakwamba wao walikuwa hawahami kutoka waliposimama kwenda katika sijida mpaka asujudu.
- Amesema Bin Daqiiq Al-Idd: Katika hilo kuna ushahidi wa utulivu wa muda mrefu kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Maamuma kwa imamu wake ana hali nne katika kumfuata: 1- Kumtangulia: Kwa kuanza kitendo kabla ya imamu wake, kwa kufika maamuma katika rukuu kabla ya imamu hajafika, mfano: Kama akirukuu kabla ya imamu, au akasujudu kabla ya imamu, na hii ni haramu, na akikusudia kumtangulia huku akijua kuwa imekatazwa kufanya hivyo basi swala yake inaharibika, sawa awe kamtangulia kutoka katika nguzo au kwenda katika nguzo, na ikiwa ni katika takbira ya kuanza swala (ile ya kuhirimia swala) basi swala yake haitokubalika, na itamlazimu arudie upya swala yake. 2- Kwenda naye sawa, aende sawa na imamu, arukuu pamoja na rukuu yake na asujudu na sijida yake, na anyanyuke pamoja na kunyanyuka kwake, na kitendo hiki kwa uchache kabisa ni machukizo, na uwazi wa dalili unaonyesha kuwa ni haramu pia; na akienda sawa na imamu katika takbira ya kuanza swala, swala yake haitokubalika na atalazimika kurudia swala yake. 3- Kumfuata: Kwa kuleta vitendo vya swala baada ya imamu wake, pasina kuchelewa, na hii ndio namna bora na ya kisheria. 4- Kwenda kinyume naye, kwa kwenda kinyume na imamu wake kiasi ambacho kinamtoa katika kumfuata, kama imamu kurukuu na akabakia maamuma kasimama mpaka imamu akakaribia kunyanyuka kutoka katika rukuu, na hii ni kinyume na sheria na ni haramu, isipokuwa ikiwa ni kwa sababu ya maradhi au utu uzima.
Ufafanuzi: العربية
يخبر البراء ابن عازب رضي الله عنه وهو صادق، أن النبي صلى الله عليه وسلم كان إذا رفع رأسه من الركوع وقال: سمع الله لمن حمده، لم يزل من خلفه قيامًا، ولم يثنِ أحدٌ ظهره للسجود حتى يضع صلى الله عليه وسلم جبهته على الأرض، ثم يقعون سجودًا بعده.
- صفة متابعة الصحابة للرسول صلى الله عليه وسلم في الصلاة، وأنهم لا ينتقلون من القيام إلى السجود حتى يسجد.
- قال ابن دقيق العيد: في ذلك دليل على طول الطمأنينة من النبي صلى الله عليه وسلم.
- للمأموم مع إمامه أربع حالات من حيث الاقتداء: 1- مسابقة: بأن يبدأ بالشيء قبل إمامه، بأن يصل المأموم إلى الرُّكن قبل أن يصل إليه الإمام، مثل: أن يركع قبل ركوع الإمام، أو يسجد قبل سجود الإمام، وهذا حرام، وإذا تعمَّد السبق مع عِلْمه بالنهي فإنَّ صلاته تبطل، سواء سبقه بركن أو سبقه إلى الركن، وإذا كان في تكبيرة الإحرام لم تنعقد صلاته، ويجب عليه أن يعيدَ الصلاة من جديد. 2- موافقة: بأن يكون موافقًا للإمام، يركع مع ركوعه ويسجد مع سجود وينهض مع نهوضه، وهذا أقلُّ أحواله الكراهة، وظاهر الأدلة أنَّها محرَّمة أيضًا؛ وإذا وافقَ الإمامَ في تكبيرة الإحرام لم تنعقِد صلاتُه وعليه الإعادة. 3- متابعة: بأن يأتي بأفعال الصلاة بعد إمامه بدون تأخُّر، وهذا هو المشروع والموافق للسُّنَّة. 4- تخلُّف: بأن يتخلَّف عن إمامه تخلُّفًا يُخرِجه عن المتابعة، كأن يركع الإمام ويبقى المأموم قائمًا إلى أن يقرب الإمام من الرفع من الرُّكوع، وهذا خلاف المشروع، وهو حرام، إلا إن كان من عذر كمرض وكبر.