Hadithi

Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَجْوَدَ النَّاسِ، وَكَانَ أَجْوَدُ مَا يَكُونُ فِي رَمَضَانَ حِينَ يَلْقَاهُ جِبْرِيلُ، وَكَانَ يَلْقَاهُ فِي كُلِّ لَيْلَةٍ مِنْ رَمَضَانَ فَيُدَارِسُهُ القُرْآنَ، فَلَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَجْوَدُ بِالخَيْرِ مِنَ الرِّيحِ المُرْسَلَةِ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili, na alikuwa akikutana naye katika kila usiku wa Ramadhani akimsomesha Qur'ani, basi hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na Amani ziwe juu yake- ni mkarimu zaidi kwa mambo ya kheri kuliko hata upepo uliotumwa.

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mkarimu zaidi kuliko watu wote katika mwezi wa Ramadhani, kiasi ambacho alikuwa akitoa kinachostahiki kumpa anayestahiki, na sababu ya kuzidisha ukarimu huu ni mambo mawili: La kwanza: Ni kukutana kwake na Jibril amani iwe juu yake. Na jambo jingine: Ni kuirejea Qur'ani, nayo ni kuisoma pasina kutazama mahali ilipoandikwa. Kwa hiyo Jibril, amani iwe juu yake, alisoma naye kila kilichoteremshwa katika Qur'ani, na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu zaidi, na ni mtenda kheri zaidi, na ni mwepesi wa kunufaisha viumbe kuliko upepo mzuri anaoutuma Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mvua na rehema.

Mafunzo

  • Kumebainishwa ukarimu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na upana wa ukarimu wake hasa katika mwezi wa Ramadhani, kwani ni mwezi wa utiifu na misimu ya matendo mema.
  • Himizo la ukarimu kila wakati, na ni sunna kuzidisha zaidi katika mwezi wa Ramadhani.
  • Kukithirisha utoaji wa misaada na ihsani na kusoma Qur'ani katika mwezi wa Ramadhani.
  • Katika sababu za kuihifadhi elimu ni kujisomea pamoja na wanafunzi wengine na wanachuoni.
Ufafanuzi: العربية

كَانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أعظم الناس كَرمًا، وكان يَكثر كرمُه في شهر رمضان حيث كان يُعطي ما ينبغي لمَن ينبغي، والسبب في زيادة كرمه أمران: الأول: الْتِقاؤه بجبريل عليه السلام. والأمر الآخر: مدارسة القرآن، وهو القراءة عن ظهر قلب. فيدارسه جبريل عليه السلام جميع ما نزل من القرآن، ولَرَسُول الله صلى الله عليه وسلم أكرم وأكثر عطاءً وفعلًا للخير، وأسرع نفعًا للخلق من الريح الطيبة التي يرسلها الله بالغيث والرحمة.

  • بيان جُود النبي صلى الله عليه وسلم وسَعَة كرمه وخاصة في رمضان، فإنه شهر الطاعات ومواسم الخيرات.
  • الحث على الجود في كل وقت، وتستحب الزيادة في شهر رمضان.
  • الإكثار من البذل والعطاء والإحسان وقراءة القرآن في شهر رمضان.
  • من أسباب حفظ العلم مدارسته مع طلاب العلم والعلماء.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi