Hadithi

Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ إِبرَاهِيمَ النَّخَعِيِّ عَنْ هَمَّامِ بنِ الحَارِثِ قَالَ: بَالَ جَرِيرٌ، ثُمَّ تَوَضَّأَ، وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ، فَقِيلَ: تَفْعَلُ هَذَا؟ فَقَالَ: نَعَمْ، رَأَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَالَ، ثُمَّ تَوَضَّأَ وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ. قَالَ الأَعْمَشُ: قَالَ إِبْرَاهِيمُ: كَانَ يُعْجِبُهُمْ هَذَا الحَدِيثُ؛ لِأَنَّ إِسْلَامَ جَرِيرٍ، كَانَ بَعْدَ نُزُولِ المَائِدَةِ.

Tafsiri

Kutoka kwa Ibrahim Nakhai kutoka kwa Hammamu bin Harithi amesema: Alikwenda haja ndogo Jariri kisha akatia udhu, na kafuta juu ya khufu zake, wakasema: Kwa nini unafanya hivi? Akasema: Ndio, Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake. Amesema A'mashi: Amesema Ibrahimu: Ilikuwa ikiwashangaza sana hadithi hii; kwa sababu kusilimu kwa Jariri kulikuwa baada ya kuteremka Suratul-Maaida.

Ufafanuzi

Alikidhi haja ndogo Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake kisha akatawadha, na akatosheka na kufuta juu ya khofu zake na hakuosha miguu yake, wakasema kumwambia walioko nao: Mbona unafanya hivi?! Akasema: Ndio, nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatawadha na akafuta juu ya khofu zake. Na Jariri alisilimu kwa kuchelewa baada ya kuteremka kwa suratul-Maaida ambayo ndani yake ina aya ya udhu, akiashiria kuwa kufuta juu ya khufu hakukufutwa kwa aya hiyo.

Mafunzo

  • Pupa ya Maswahaba na wanafunzi wao ya kufuata sunna ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  • Amesema Nawawi: Wamekubaliana wanaozingatiwa makubaliano yao juu ya kufaa kufuta juu ya khufu mbili, safarini na nyumbani, sawa sawa iwe kwa haja au bila haja, mpaka inafaa kwa mwanamke alioko nyumbani kwake na mgonjwa asiyeweza kutembea.
  • Ubora wa Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, kiasi kwamba alikuwa na kifua kipana, akistahamili kukemewa na wanafunzi wake, hata kama wamekosea katika hilo.
  • Kumjibu mwenye kukataa kufuta juu ya khufu mbili na akadai kuwa kulifutwa; kwa sababu hadithi ya Jariri radhi za Allah ziwe juu yake imechelewa kuliko aya ya udhu.
  • Kumebainishwa kwamba ni lazima kwa mwenye kukemewa jambo na akawa akiitakidi usahihi wake asimkasirikie anayemkemea, bali ajadiliane naye kulingana na dhana yake, bali ambainishie hoja yake katika hilo kwa majibu mazuri.
  • Kutoa ushihidi kupitia historia wakati wa haja ya kufanya hivyo.
Ufafanuzi: العربية

بال جرير بن عبد الله رضي الله عنه ثم توضأ، واكتفى بالمسح على خُفَّيه ولم يغسل رجليه، فقال له مَن حوله: تفعل هذا؟! فقال: نعم، رأيت النبي صلى الله عليه وسلم بال، ثم توضأ ومسح على خفيه. وكان جرير قد أسلم متأخِّرًا بعد نزول سورة المائدة التي فيها آية الوضوء، مشيرًا بذلك إلى أن المسح على الخفين لم يُنسخ بتلك الآية.

  • حرص الصحابة والتابعين على اتباع سنة النبي صلى الله عليه وسلم.
  • قال النووي: أجمع من يُعتدُّ به في الإجماع على جواز المسح على الخفين، في السفر والحضر، سواء كان لحاجة أو لغيرها، حتى يجوز للمرأة الملازمة بيتها والزَّمِن الذي لا يمشي.
  • فضل جرير بن عبد الله رضي الله عنه حيث كان واسع الصدر، يتحمل إنكار طلابه عليه، وإن كانوا مخطئين في ذلك.
  • الرد على من أنكر المسح على الخفين وادعى بأنه منسوخ؛ لأن حديث جرير رضي الله عنه متأخر عن آية الوضوء.
  • بيان أنه ينبغي لمن أنكر عليه شيء، وكان يعتقد صحته ألَّا يغضب على من ينكر عليه، ويناقشه بحسب ظنه، بل يبين له مستنده في ذلك بالتي هي أحسن.
  • الاستدلال بالتاريخ عند الحاجة إليه.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi