Hadithi

Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ لِبِلاَلٍ عِنْدَ صَلاَةِ الفَجْرِ: «يَا بِلاَلُ، حَدِّثْنِي بِأَرْجَى عَمَلٍ عَمِلْتَهُ فِي الإِسْلاَمِ، فَإِنِّي سَمِعْتُ دَفَّ نَعْلَيْكَ بَيْنَ يَدَيَّ فِي الجَنَّةِ» قَالَ: مَا عَمِلْتُ عَمَلًا أَرْجَى عِنْدِي أَنِّي لَمْ أَتَطَهَّرْ طَهُورًا، فِي سَاعَةِ لَيْلٍ أَوْ نَهَارٍ، إِلَّا صَلَّيْتُ بِذَلِكَ الطُّهُورِ مَا كُتِبَ لِي أَنْ أُصَلِّيَ.

Tafsiri

kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema kumwambia Bilali wakati wa swala ya Alfajiri: "Ewe Bilali, hebu nihadithie kuhusu amali yenye matarajio makubwa zaidi uliyowahi kuifanya ndani ya Uislamu, kwani mimi nilisikia mkanyago wa viavu vyako mbele yangu huko Peponi" Akasema: Sijawahi kufanya amali yoyote yenye matarajio kwangu isipokuwa sijawahi kutia udhu wowote, katika nyakati za usiku au mchana, isipokuwa ninaswali kwa udhu huo kiasi nilichoandikiwa niswali katika rakaa.

Ufafanuzi

Aliona Mtume rehema na amani ziwe juu yake usingizini kuwa yuko Peponi, akasema kumwambia Bilal bin Rabaha: Nieleze kuhusu amali yoyote ya sunna yenye matarajio makubwa uliowahi kuifanya ndani ya Uislamu? kwani mimi nilisikia sauti ya chini ya viatu vyako wakati wa kuvitikisa kwa kutembea mbele yangu Peponi. Bilal akasema: Sikuwahi kufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa yoyote kwangu zaidi yakuwa sijawahi kutengukwa udhu wakati wowote iwe usiku au mchana isipokuwa ninatawadha, kisha ninaswali kwa ajili ya Mola wangu kwa udhu huo swala za sunna zisizo na mpaka kiasi nilichoandikiwa kuswali.

Mafunzo

  • Ubora wa amali aliyoisema Bilal radhi za Allah ziwe juu yake, nayo ni swala kila anapopata twahara na akatia udhu, na kwamba hiyo ni miongoni mwa amali inayotarajiwa zaidi, na ni sababu ya kuingia Peponi.
  • Sunna ya kuswali baada ya kila udhu.
  • Kiigizo na mlezi kuuliza matendo ya mwanafunzi wake; ili amhimize kudumu nayo kama ni matendo mazuri, na kama si hivyo basi amkataze.
  • Ushahidi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Bilal radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ni katika watu wa peponi.
  • Swali hili lilikuwa wakati wa swala ya Alfajiri, na kwa hili ni ishara kuwa tukio hili lilitokea katika ndoto yake rehema na amani ziwe juu yake, na ndoto za Manabii ni kweli.
Ufafanuzi: العربية

رأى النبي صلى الله عليه وسلم في المنام أنه في الجنة، فقال لبلال بن رباح: أخبرني بأرجى عملِ تطوعٍ عملته في الإسلام؟ فإني سمعت صوتًا خفيفًا لنعليك عند تحريكهما بالمشي أمامي في الجنة. قال بلال: ما عملت عملًا أرجى عندي أني لم أحدث في ساعة ليل أو نهار إلا وتوضأت، ثم صليت لربي بذلك الوضوء من النوافل المطلقة ما كتب لي أن أصلي.

  • فضل العمل الذي دل عليه بلال رضي الله عنه، ألا وهو الصلاة كلما تطهر وتوضأ، وأنه من أرجى الأعمال وسبب لدخول الجنة.
  • استحباب الصلاة بعد كل وضوء.
  • سؤال القدوة أو المربي عن عمل تلميذه؛ ليحضَّه على الثبات عليه إن كان حسنًا، وإلا فينهاه.
  • شهادة من النبي صلى الله عليه وسلم لبلال رضي الله عنه بأنه من أهل الجنة.
  • هذا السؤال عند صلاة الفجر، وفي هذا إشارة إلى أن ذلك وقع في رؤيا منام منه صلى الله عليه وسلم، ورؤيا الأنبياء حق.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi