Hadithi

Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: وُقِّتَ لَنَا فِي قَصِّ الشَّارِبِ، وَتَقْلِيمِ الْأَظْفَارِ، وَنَتْفِ الْإِبِطِ، وَحَلْقِ الْعَانَةِ، أَلَّا نَتْرُكَ أَكْثَرَ مِنْ أَرْبَعِينَ لَيْلَةً.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Tuliwekewa muda wa kupunguza sharubu, na kupunguza kucha, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, tusiziache zaidi ya siku arobaini.

Ufafanuzi

Aliweka kikomo Mtume rehema na amani ziwe juu yake cha mtu kupunguza sharubu, na kupunguza kucha za mikono na miguu, na kung'oa nywele za kwapa, na kunyoa nywele za siri, kusizidi kuziacha kwake zaidi ya siku arobaini.

Mafunzo

  • Amesema Shaukani: Kilicho sawa nikuwa adhibiti kwa arobaini aliyoidhibiti kwayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake haitakiwi kuivuka, na haitochukuliwa kama kwenda kinyume na sunna kwa kuacha kupunguza na mfano wake baada kurefuka mpaka ifike kikomo cha muda huo.
  • Amesema bin Hubaira: Hadithi hii ndio kikomo cha kuchelewesha hilo, na kilichobora ni kulitekeleza hilo kabla ya ukomo huo.
  • Uislamu umetilia kipaumbele usafi na kujitwaharisha na kujipamba.
  • Kupunguza sharubu, kwa kunyoa nywele zinazoota juu ya mdomo wa juu.
  • Kukwapua nywele za kwapa, kwa kuondoa nywele zinazoota humo, nayo ni sehemu inayokuwa chini ya maungio kati ya mkono na bega.
  • Kunyoa nywele za siri, nazo ni nywele zinazoota pembezoni mwa tupu ya mbele, kwa mwanaume na mwanamke.
Ufafanuzi: العربية

حَدَّد النبي صلى الله عليه وسلم لقَصّ شارب الرجل، وقص أظفار الأيدي والأرجل، ونتف الإبط، وحلق العانة، بأن لا يزيد تركها عن أربعين يومًا.

  • قال الشوكاني: المختار أنه يُضبَط بالأربعين التي ضبط بها رسول الله صلى الله عليه وسلم فلا يجوز تجاوزها، ولا يُعدّ مخالفًا للسنة من ترك القص ونحوه بعد الطول إلى انتهاء تلك الغاية.
  • قال ابن هبيرة: هذا الحديث هو الغاية في تأخير ذلك، والأولى أخذ ذلك فيما قبل هذه الغاية.
  • عناية الإسلام بالنظافة والتطهر والزينة.
  • قص الشارب، بأخذ بعض الشعر النابت على الشفة العليا.
  • نتف الإبط، بإزالة الشعر الذي يَنبُت به، وهو الموضع الذي يكون أسفل مِفْصَل الذراع بالكتف.
  • حلق شعر العانة، وهو الشعر الخَشِن النابت حول القُبُل، من الرجل والمرأة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi