Hadithi

Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Al-Bukhaariy

Matini ya Kiarabu

عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ رَجُلًا عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ اسْمُهُ عَبْدَ اللَّهِ، وَكَانَ يُلَقَّبُ حِمَارًا، وَكَانَ يُضْحِكُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ جَلَدَهُ فِي الشَّرَابِ، فَأُتِيَ بِهِ يَوْمًا فَأَمَرَ بِهِ فَجُلِدَ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ القَوْمِ: اللَّهُمَّ الْعَنْهُ، مَا أَكْثَرَ مَا يُؤْتَى بِهِ؟ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَلْعَنُوهُ، فَوَاللَّهِ مَا عَلِمْتُ أَنَّهُ يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba mtu mmoja alikuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake jina lake anaitwa Abdallah, na alikuwa akitaniwa kwa jina la Punda, na alikuwa akimchekesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa viboko kwa sababu ya ulevi, basi akaletwa siku moja akaamrisha akachapwa, akasema mtu mmoja katika jamaa waliopo: Ewe Mwenyezi Mungu mlaani, ni mara ngapi analetwa!? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

Ufafanuzi

Katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa na bwana mmoja jina lake Abdallah, na akiitwa Punda, kwa jina la utani, na alikuwa akimchekesha sana Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika baadhi ya maneno yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa kwa sababu ya kunywa pombe, siku moja akaletwa tena akiwa amekunywa pombe, akaamrisha akachapwa. Mmoja kati ya waliopo akamtukana, na akasema: Mwenyezi Mungu mlaani, amezidi sana kuletwa kwa sababu ya kunywa pombe?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Msimuombee kufukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, na Wallahi sijajua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume.

Mafunzo

  • Haipingani kati ya kufanya makatazo na kuthibiti kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndani ya moyo wa mwenye kuyafanya; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa huyo aliyetajwa katika hadithi anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na hayo yaliyojitokeza kwake.
  • Mtenda madhambi makubwa atakapokufa na huku anaendelea na chochote katika hayo huyo atakuwa chini ya matashi, akitaka Mwenyezi Mungu atamsamehe na akitaka atamuadhibu, na habakishwi milele motoni yeyote katika Waislamu.
  • Inachukiza kumlaani mnywa pombe; kwa kutaraji kuwa huenda kukawa na kizuizi cha kutompata laana; kwa sababu kumlaani mtu maalumu na kumuombea dua mbaya, huenda hilo likampelekea katika ujeuri, au likamkatisha tamaa ya kukubaliwa toba.
  • Inafaa kulaani bila kumuanisha mtu kwa hilo.
Ufafanuzi: العربية

كان على عهد النبي صلى الله عليه وسلم رجل اسمه عبد الله، ويلقب حمارًا، كان يضحك النبي صلى الله عليه وسلم في بعض كلامه، وكان صلى الله عليه وسلم قد جلده في شرب الخمر، فأتي به يوما قد شرب الخمر فأمر به فجلد. فسبه أحد الحاضرين، وقال: لعنه الله، ما أكثر ما يؤتى به قد شرب الخمر؟! فقال صلى الله عليه وسلم: لا تدعوا عليه بالطرد من رحمة الله، فوالله ما علمت إلا أنه يحب الله ورسوله.

  • لا تنافي بين ارتكاب النهي وثبوت محبة الله ورسوله في قلب المرتكب له؛ لأنه صلى الله عليه وسلم أخبر أن المذكور يحب الله ورسوله مع ما صدر منه.
  • مرتكب الكبيرة إذا مات وهو مصِرٌّ على شيء منها فهو تحت المشيئة، إن شاء الله غفر له وإن شاء عذبه، ولا يخلَّد في النار أحد من أهل الإسلام.
  • كراهة لعن شارب الخمر المعين؛ لاحتمال قيام مانع من لحوق اللعن؛ ولأن لعن المعين والدعاء عليه قد يحمله على التمادي، أو يُقنِّطه من قبول التوبة.
  • جواز لعن غير المعين المتصف بذلك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi