Hadithi

Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قَالَ: مَرَّ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِقَبْرَيْنِ، فَقَالَ: «إِنَّهُمَا لَيُعَذَّبَانِ، وَمَا يُعَذَّبَانِ فِي كَبِيرٍ، أَمَّا أَحَدُهُمَا فَكَانَ لاَ يَسْتَتِرُ مِنَ البَوْلِ، وَأَمَّا الآخَرُ فَكَانَ يَمْشِي بِالنَّمِيمَةِ» ثُمَّ أَخَذَ جَرِيدَةً رَطْبَةً، فَشَقَّهَا نِصْفَيْنِ، فَغَرَزَ فِي كُلِّ قَبْرٍ وَاحِدَةً، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، لِمَ فَعَلْتَ هَذَا؟ قَالَ: «لَعَلَّهُ يُخَفِّفُ عَنْهُمَا مَا لَمْ يَيْبَسَا».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, akasema: "Hakika hao wawili wanaadhibiwa, na hawaadhibiwi kwa makosa makubwa, ama mmoja wao alikuwa hajistiri na mkojo, na ama mwingine alikuwa akitembea kwa kuchonganisha watu" Kisha akachukua kuti bichi, akalikata vipande viwili, akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa nini umefanya hivi? Akasema: "Huenda yakawapunguzia kinachowapata kwa muda kabla hayajakauka".

Ufafanuzi

Alipita Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili akasema: Hakika watu wa makaburi haya mawili wanaadhibiwa; na wala hawaadhibiwa katika jambo kubwa, hata kama ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu, Ama mmoja wao alikuwa hajali katika kuhifadhi mwili wake na nguo zake kutokana na mkojo anapokidhi haja yake, Na mwingine alikuwa akitembea kati ya watu kwa uchonganishi, akinukuu maneno ya mtu mwingine kwa lengo la kuwadhuru na kuleta sintofahamu baina yao na ugomvi kati ya watu.

Mafunzo

  • Uchonganishi na kuacha kujistiri na mkojo ni katika madhambi makubwa na ni katika sababu za adhabu za kaburini.
  • Mwenyezi Mungu Mtukufu alifunua baadhi ya mambo yaliyofichikana kama adhabu za kaburini ili kuonyesha alama ya utume wake rehema na amani ziwe juu yake.
  • Kitendo hiki cha kuchukua tawi na kulipasua vipande viwili na kuviweka juu ya makaburi ni maalumu kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu alimfunulia kuona hali za watu wa makaburi yale mawili, hakiwezi kuwa kipimo cha watu wengine, kwa sababu hakuna ajuaye hali za watu walioko kaburini.
Ufafanuzi: العربية

مَرَّ النبيُّ صلى الله عليه وسلم بقبرين فقال: إنَّ صاحبَي هذين القبرين لَيُعذّبان؛ وما يعذبان في أمر كبير في نظركم، وإن كان كبيرًا عند الله، أمّا أحدُهما فكان لا يَهتَمُّ بحفظ جَسَدِه وثيابِه مِن البول حين يَقْضي حاجتَه، والآخَرُ كان يمشي بالنميمة بين الناس، فيَنْقُلُ كلامَ غيرِه بقصد الإضرار وإيقاع الخلاف والوقيعة بين الناس.

  • النميمةُ وتركُ التنزُّهِ مِن البول مِن كبائر الذنوب ومِن أسباب عذاب القبر.
  • كَشف الله سبحانه بعض المغيبات -كعذاب القبر- إظهارًا لعلامة نبوتِهِ صلى الله عليه وسلم.
  • هذا الفعلُ مِن شَقِّ الجريدتين ووضعِها على القبر خاصٌّ بالنبي صلى الله عليه وسلم؛ لأن الله أطْلَعَه على حالِ صاحبَي القبر، فلا يقاس غيره به لأنه لا أحد يعلم أحوال أصحاب القبور.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi