Hadithi

“Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.”

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْها أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: «لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ اليَوْمَ مِنْ رَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذِهِ» وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِ الإِبْهَامِ وَالَّتِي تَلِيهَا، قَالَتْ زَيْنَبُ بِنْتُ جَحْشٍ فَقُلْتُ يَا رَسُولَ اللَّهِ: أَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: «نَعَمْ إِذَا كَثُرَ الخَبَثُ».

Tafsiri

Kutoka kwa Zainab bint Jahshi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliingia ndani kwake akiwa na mfadhaiko huku akisema: “Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, ole wao waarabu na watahadhari dhidi ya shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya'juuju na Ma'ajuju upenyo wa kiasi hiki.” Jahshi akasema: Basi nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu: Je, tuangamie na hali miongoni mwetu wamo watu wema? Akasema: "Ndio, ikiwa maovu yatakithiri".

Ufafanuzi

Aliingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Zainab bint Jahshi Mwenyezi Mungu amuwie radhi, akiwa na mfadhaiko na khofu kubwa, akasema: Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, akiashiria kutaraji jambo baya litatokea, na hakuna kusalimika katika hilo ila kwa kurejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kisha akasema: Ole wao Waarabu kutokana na shari inayokaribia kutokea, leo imefunguliwa katika ngome ya Ya'ajuj na Ma'ajuj kiasi hiki, ambacho ni ukuta alioujenga Dhul-Qarnain, na akazungusha duara kwa kidole gumba chake na kile kinachofuata (kuonyesha kiasi kilicho funguliwa). Akasema Zainab Mwenyezi Mungu amuwie radhi: Vipi Mwenyezi Mungu atuangamize na hali wapo waumini wema miongoni mwetu? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: “Maovu yatakapokithiri, kama vile uovu, ufisadi, maasi, uzinzi, pombe na vitu vingine, maangamizo yatawakumba wote.

Mafunzo

  • Hofu haiushughulishi moyo wa muumini kiasi cha kuacha kumtaja Mwenyezi Mungu wakati wa hofu, kwa sababu kwa kumtaja Mwenyezi Mungu mioyo hupata utulivu.
  • Himizo la kukemea maasi na kuzuia kutokea kwake.
  • Maangamizo ya watu wote hutokea kwa sababu ya kukithiri kwa maasi na kuenea kwake, na kutoyakemea hata kama watu wema ni wengi.
  • Majanga huwakumba watu wote, wema na waovu, lakini wao watafufuliwa kulingana na nia zao.
  • "Amewataja Waarabu katika kauli yake: "Ole wao Waarabu kwa shari iliyokaribia"; kwa sababu wao ndio walioingia katika Uislamu kwa wingi wakati akisema hivyo.
Ufafanuzi: العربية

دَخَلَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على زينب بنت جَحْش رضي الله عنها فَزِعًا خائفًا، وهو يقول: لا إله إلا الله، إيذانًا بتوقُّع أمرٍ مكروهٍ يَحْدُث، ولا نجاة منه إلا بالالتجاء إلى الله سبحانه، ثم قال صلى الله عليه وسلم: ويل للعرب من شر قد اقترب وقوعُه، فُتِح اليوم من رَدم يأجوج ومأجوج، وهو السَّدُّ الذي بناه ذو القرنين، مثل هذه، وحَلَّق بإصبعه الإبهام والتي تليها، فقالت زينب رضي الله عنها: كيف يُسلِّط الله علينا الهلاك وفينا المؤمنون الصالحون؟ فقال لها النبي صلى الله عليه وسلم: إذا كَثُرَ الخَبَث مِن الفسوق والفجور والمعاصي، والزنا، والخمور، وغيرها، عَمَّ الهلاكُ الجميع.

  • الفَزَع لا يشغل قلبَ المؤمن عن ذكر الله عند الخوف؛ لأنه بذكر الله تطمئن القلوب.
  • الحث على إنكار المعاصي ومنع وقوعها.
  • يحصل الهلاك العامُّ بسبب كثرة المعاصي وانتشارها وعدم إنكارها وإن كثر الصالحون.
  • المصائب تعمُّ الناس جميعًا صالحين وفاسدين، ولكنهم يُبعَثون على نيّاتهم.
  • خصَّ العربَ في قوله: "وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ"؛ لأنهم مُعظم مَن أَسْلَم حين قال ذلك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi