Hadithi

Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضيَ اللهُ عنهما: أنَّهُ قَالَ لعَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ: أَلَا أُرِيكَ امْرَأَةً مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هَذِهِ الْمَرْأَةُ السَّوْدَاءُ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: إِنِّي أُصْرَعُ وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ، فَادْعُ اللهَ لِي، قَالَ: «إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ أَنْ يُعَافِيَكِ» قَالَتْ: أَصْبِرُ، قَالَتْ: فَإِنِّي أَتَكَشَّفُ فَادْعُ اللهَ أَنْ لَا أَتَكَشَّفَ، فَدَعَا لَهَا.

Tafsiri

Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.

Ufafanuzi

Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo

  • Subira juu ya mabalaa katika dunia hupelekea kupata Pepo.
  • Amesema Nawawi: Na hapa kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa kuanguka kwa mtu hulipwa malipo yaliyokamilika
  • Tazama heshima na haya kwa wanawake wa kiswahaba, na pupa yao juu ya kujisitiri, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, mwanamke huyu, kubwa zaidi alilokuwa akilihofia ni kufunuka sehemu ya mwili wake.
  • Amesema bin Hajari: Kuchukua jambo gumu ni bora kuliko kuchukua ruhusa, kwa mtu atakayejua kuwa anauwezo wa kulibeba, na hatodhoofika kwa kulibeba gumu hilo.
  • Amesema bin Hajari: Na hapa nikuwa; tiba ya maradhi yote ni kwa dua na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hufaa zaidi na kunufaisha zaidi kuliko tiba ya miti shamba (madawa), na kwamba athari ya hilo na muitikio wa mwili ni mkubwa zaidi kuliko athari ya dawa za mwili, lakini huleta ahueni kwa mambo mawili: La kwanza: Upande wa mgonjwa, kuwa na imani ya kweli na Mwenyezi Mungu, na la pili: Upande wa tabibu, kuwa na nguvu kubwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa na nguvu kubwa ya uchamungu, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi.
  • Amesema bin Hajari: Hapa kuna ushahidi juu ya kuacha kutumia dawa.
Ufafanuzi: العربية

قال ابن عباس رضي الله عنهما لعطاء بن أبي رباح: ألا أريك امرأة من أهل الجنة؟ قال عطاء: بلى، قال: هذه المرأة الحبشية السوداء، أتت النبي صلى الله عليه وسلم، قالت: إن بي مرض فأصرع وإني أتكشف ويظهر شيء من جسدي وأنا لا أشعر، فادع الله أن يعافيني، قال: إن شئت صبرت ولك الجنة، وإن شئت دعوت الله أن يعافيك، قالت: أصبر إذن، ثم قالت: فادع الله أن لا أتكشف إن صرعت، فدعا الله لها.

  • الصبر على البلاء في الدنيا يورث الجنة.
  • قال النووي: وفيه دليل على أن الصرع يثاب عليه أكمل ثواب.
  • عفة وحياء نساء الصحابة، وحرصهن على الستر، رضي الله عنهن، فهذه المرأة كانت أكثر ما تخشاه أن ينكشف شيءٌ من جسمها.
  • قال ابن حجر: أن الأخذ بالشدة أفضل من الأخذ بالرخصة لمن علم من نفسه الطاقة ولم يضعف عن التزام الشدة.
  • قال ابن حجر: وفيه أن علاج الأمراض كلها بالدعاء والالتجاء إلى الله أنجع وأنفع من العلاج بالعقاقير، وأن تأثير ذلك وانفعال البدن عنه أعظم من تأثير الأدوية البدنية، ولكن إنما ينجع بأمرين: أحدهما من جهة العليل وهو صدق القصد، والآخر من جهة المداوي، وهو قوة توجهه وقوة قلبه بالتقوى والتوكل، والله أعلم.
  • قال ابن حجر: فيه دليل على جواز ترك التداوي.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi